Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 17 Rabi' I 1447 | Na: H 1447 / 10 |
M. Jumanne, 09 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani ya Kibeberu Inatumia Wakala Wake Shirika la Excelerate Energy kutia Udhibiti juu ya Bandari na Bahari zetu za Kimkakati ili Kuendeleza Udhibiti wake wa Kisiasa
(Imetafsiriwa)
Balozi wa zamani wa Marekani nchini Bangladesh Peter D Haas alifanya mkutano wa karibu saa moja na Waziri wa Mambo ya Nje Asad Alam Siam mnamo Alhamisi (4 Septemba). Ingawa hakuna upande uliofichua maelezo ya majadiliano hayo, vyanzo vya habari viliripoti kuwa mazungumzo hayo yalihusu uwezekano wa kuagiza LNG kutoka Marekani, pamoja na ushirikiano wa sasa na miradi ya mustakabali. Kwa sasa Haas anatumika kama Mshauri wa Kimkakati wa Excelerate Energy - shirika la kimataifa la Texas ambalo linaendesha kituo cha LNG kinachoelea huko Maheshkhali, Cox’s bazar. Ina mipango ya kujenga kituo chengine cha LNG huko Payra, Patuakhali katika siku zijazo. Haas amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje kama mwakilishi wake jijini Dhaka. Kampuni kama Excelerate Energy zinacheza dori muhimu katika kuendeleza ushawishi wa kijiografia wa Marekani, ambao unalingana kikamilifu na Mkakati wa Indo-Pacifiki (IPS). Huu ni ‘ubeberu laini’ imara na wa kisasa ambao Marekani inadhihirisha kupitia ufundi wa kiuchumi. Marekani sasa inapata ushawishi wa kimataifa si kupitia uvamizi wa kikoloni wa mtindo wa karne ya 18; badala yake, inatumia zana kama vile mikataba ya nishati kuunda mfumo wa kutegemeana ambapo mataifa kwa hiari yanapatana na maslahi ya kijiografia ya Marekani. Na mfumo huu wa kimataifa unahakikisha kwamba njia muhimu za baharini na sehemu za kuchomoa za siasa za kijiografia hatimaye zinalindwa na mamlaka ya Marekani. Kwa hivyo, mikataba ya nishati na Marekani zinahusu zaidi ya kukabidhi tu miundombinu yetu ya nishati na kuweka ubwana wetu wa kiuchumi hatarini. Sio tu suala la kutishia usalama wetu wa nishati kwa kuunda utegemezi wa kudumu kwa LNG iliyoagizwa kutoka nje na ya gharama kubwa. Badala yake, zaidi ya hayo, Marekani itafungua njia za baharini kwa nchi zinazotegemea uagizaji wa nishati, kama vile Bangladesh na Pakistan. Hatimaye, Bangladesh itategemea mfumo wa usalama wa baharini unaoongozwa na Marekani kwa mahitaji yake ya nishati. Uthabiti wetu wa kiuchumi utategemea usalama ambao Marekani hutoa ili kudumisha udhibiti wake.
Eneo kuu la Bangladesh ndio sababu imekuwa uwanja muhimu wa vita kwa Marekani kudumisha ukuu wake wa kimataifa katika eneo hilo. Ghuba ya Bengal ni ukumbi muhimu wa kimkakati, unaozunguka eneo muhimu la unyongaji, Mlango Bahari wa Malacca, na inayoangazia njia kuu za usambazaji wa nishati za China. Kwa hivyo, Marekani tayari imetumia wakala wake mwenye uwezo mkubwa zaidi katika eneo hilo, Japan, kuwekeza katika bandari ya bahari kuu ya Matarbari ya Bangladesh. Bandari hii inaweza kubeba meli kubwa, kipengee muhimu cha kimkakati. Katika siku zijazo, inaweza kusaidia meli za nevi kutoka Japan, Marekani, India, na washirika wengine wa Quad. Hili linatumikia malengo mapana zaidi ya maslahi ya kimkakati ya Marekani kwanza kwa gharama yetu wenyewe.
Enyi Watu! Tunakuonyeni juu ya hatari inayokuja kwa ubwana wetu na mustakabali wetu. Hatari hiyo ni nguvu isiyodhibitiwa ya ubeberu ya Marekani, ambayo haiwasili na wanajeshi wake kwenye ufuo wetu wakipeperusha bendera ya Marekani. Inawasili na mikataba ya nishati katika sekretarieti zetu. Ni ya siri zaidi, na, kwa hiyo, ni hatari zaidi. Inatoa mwonekano wa ushirikiano lakini inachukua fursa ya bandari zetu za kimkakati na bahari, na kudhoofisha ubwana wetu. Haishangazi kwamba mikataba hii kutoka Marekani inanunua kimya cha kipote cha mabepari wa nchi yetu na wanasiasa wafisadi. Lakini kinachotia wasiwasi na kuvunja moyo ni kimya cha wanasiasa na wanafikra waaminifu tunaowafahamu, hasa tangu Mapinduzi ya Julai, kuhusu mikataba hii ya Marekani. Kimya chao ni matokeo ya Marekani kujihusisha na mashirika yetu ya kiraia na taasisi za kisiasa kwa muda mrefu, na kutoa viongozi wanaoafikiana na mtazamo wa ulimwengu wa Marekani. Bora zaidi, wanaona mikataba hii kwa mtazamo wa kiuchumi pekee, bila kufahamu ukweli kwamba kisiasa inatudogosha kuwa mteja wa kudumu wa Marekani, badala ya mshirika. Hizb ut Tahrir, Wilayah Bangladesh kwa hiyo inawaombeni msiwe tena watazamaji walio kimya kwa utiifu wetu wenyewe. Unganeni na chama chenye uwezo cha Hizb ut Tahrir ambacho kina mradi wa wazi wa kupinga utawala wa kibeberu wa Marekani. Kwa usaidizi wenu mkubwa na usioyumba, Hizb ut Tahrir iko tayari kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume iliyoahidiwa ili kukupelekeni kwenye nafasi ya nguvu ya pamoja ya kuzuia kutawaliwa na mabeberu.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ ...]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao …” [Sura An-Nur:55].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |