Afisi ya Habari
Australia
| H. 1 Jumada I 1447 | Na: 04 / 1447 H |
| M. Alhamisi, 23 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Australia Yajitolea kwa Ukaliaji wa Kimabavu wa Palestina Iliyosalia
(Imetafsiriwa)
Serikali ya Australia imetangaza kuwa itakuwa sehemu ya ‘Jopokazi la Ujenzi Mpya wa Gaza’ la Trump, muungano unaoongozwa na Marekani wa dola za Magharibi, Waarabu na Waislamu uliopewa jukumu la kuondoa silaha kwa nguvu mjini Gaza na kukabidhiwa kwake baadaye kwa umbile vamizi.
Tangazo hili linakuja huku umbile hilo vamizi pia likitangaza nia yake ya kudai uhuru juu ya Ukingo wa Magharibi pia, sambamba na juhudi pana za Marekani za kulazimisha udhibiti wa Wazayuni juu ya Palestina nzima katika jaribio lake la kuunda upya Mashariki ya Kati nzima.
Hizb ut Tahrir / Australia ingependa kusisitiza yafuatayo:
1. Australia ina rekodi ndefu ya kutumikia maslahi ya kikoloni katika Mashariki ya Kati. Hakika, ilikuwa Brigedi ya Light Horse ya Australia iliyoingia Palestina kwa mara ya kwanza wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia kwa niaba ya Waingereza, ikiwezesha uvamizi wake na vikosi vya Uingereza na baadaye kukabidhiwa kwa wavamizi wa Kizayuni.
2. Mchango wa Australia kwa ‘Kikosi cha Ujenzi Mpya wa Gaza’ umeundwa ili kusaidia kulazimisha kujisalimisha kwa Gaza kisiasa baada ya umbile vamizi kushindwa kufanya hivyo kijeshi. Australia ilitekeleza mauaji yake yenyewe ya halaiki dhidi ya watu wake wa asili, iliwezesha mauaji ya halaiki ya kwanza dhidi ya watu wa Palestina, ilisimama kimya kuhusu mauaji ya halaiki ya miaka miwili iliyopita, na sasa inalisaidia umbile vamizi kufuta kitambulisho cha Palestina milele. Australia milele italaaniwa kwa uwezeshaji wake wa jinai hizi.
3. Uhalifu mkubwa zaidi katika mkasa huu wote ni usaliti wa watawala wa Kiarabu na Waislamu. Daima wamesimama kama safu ya kwanza na ya mwisho ya ulinzi kwa uvamizi huo na wamethibitisha kwa mara nyengine tena usaliti wao kwa kukubali kupeleka vikosi vyao kusalimisha Palestina badala ya kuikomboa. Muislamu yeyote anayeendelea kupanua uhalali kwa watawala hawa, kutetea uhalifu wao au kusaidia kutekeleza usaliti wao, milele atakuwa mshirika wa uhalifu wao.
4. Muungano wa kimataifa wa Makruseda wa Kizayuni (Zio-Crusader) unaoundwa kulazimisha kujisalimisha kwa Palestina ni ukumbusho mkali wa chuki ya kihistoria iliyo ndani kabisa ambayo dola hizi zinautazama kwayo ulimwengu wa Kiislamu. Wanajiona kama urithi unaoendelea wa makruseda wa kwanza, ambao hawatakoma hadi ulimwengu wote wa Kiislamu utakapokamatwa, na Uislamu na Waislamu kushindwa kabisa.
5. Imerudiwa kwa karne iliyopita, lakini inagusa zaidi hivi sasa ... isipokuwa Waislamu watangaze utashi wao wa kisiasa, wawatupilie mbali watawala wao wasaliti na kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida, tutabaki milele chini ya uhalifu wa Makruseda wa Kizayuni (Zio-Crusaders) na usaliti wa wasaidizi wao wa ndani. Ni wakati muafaka sasa wa kuikamata mikono ya wakandamizaji, kila mahali.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Australia
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Australia |
Address & Website Tel: 0438 000 465 www.hizb-australia.org |
E-Mail: media@hizb-australia.org |