Afisi ya Habari
Australia
H. 17 Safar 1447 | Na: 01 / 1447 H |
M. Jumatatu, 11 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Utambuzi wa Kimasharti wa Serikali ya Australia wa Palestina ni Zawadi kwa Mauaji ya Halaiki, Sio Haki
(Imetafsiriwa)
Waziri Mkuu Anthony Albanese ametangaza rasmi kujiandaa kwa Australia kuitambua dola ya Palestina. Yeye binafsi aliwapigia simu Mahmoud Abbas na Benjamin Netanyahu kabla, kana kwamba kuwaridhisha wahalifu wale wale waliohusika na miongo kadhaa ya uhalifu.
Waziri Mkuu alisema hivi karibuni kutambuliwa kwa dola ya Palestina kunategemea utambuzi wa Palestina kwa uvamizi, kukubali mipaka yake ya kudumu, kuondolewa nguvu za kijeshi kwa dola ya baadaye ya Palestina na kuondolewa kabisa kwa Hamas na juhudi zozote za upinzani ilizo nazo.
Pendekezo la serikali ya Australia sio chochote zaidi ya malipo kwa mauaji ya halaiki: kutoa dola ya kindoto, isiyo na maana iliyonyang'anywa uwezo wa kujilinda, kulazimishwa kuachia ardhi yake iliyoibiwa, inayoamriwa na dola za Magharibi juu ya nani anayepaswa kuitawala na kulazimishwa kuhalalisha mahusiano na umbile halifu la kishenzi.
Haya si masharti ya haki. Haya ni malengo yale yale yanayotafutwa na umbile la Kizayuni na waungaji mkono wake wa Marekani baada ya takriban miaka miwili ya mauaji ya halaiki. Australia inatafuta tu kusaidia kuendeleza kujisalimisha kidiplomasia baada ya uvamizi huo kushindwa kupata lengo mojawapo kijeshi, kwa matumaini ndoto ya dola ya Palestina inaweza kuwa karoti ambayo inathibitisha ufanisi baada ya kutumia fimbo ya mauaji ya halaiki.
Kinaya ni kwamba Australia imetangaza hamu ya kutaka kuitambua dola ya Palestina lakini inashindwa kuwatambua Wapalestina wenyewe. Sera ya kinyama ya serikali hii ya kulaumu wahasiriwa imefanya mateso ya Wapalestina kutoonekana na jinai za wavamizi wao kutowajibishwa. Ni baada tu ya Wapalestina wengi kuuawa au kuhamishwa makaazi ambapo Australia sasa inatafuta kuitambua Palestina wakati hakuna chochote kilichosalia cha kutambuliwa.
Ulimwengu umeshtushwa na uvamizi ambao sasa unasimama kwenye ukingo wa kutunga “suluhisho la mwisho” nchini Palestina. Australia, kwa upande wake, inatafuta sana kujifanya kuwa haina hatia juu ya ushiriki wake, na kwa kufanya hivyo, imethibitisha tu hatia yake. Muungano wa Mazayuni na Magharibi umefumuka mbele ya ulimwengu, na hakuna kiasi cha maneno ya kejeli au ishara kitakachoweza kuficha uhalisia wake mbaya.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Australia |
Address & Website Tel: 0438 000 465 www.hizb-australia.org |
E-Mail: media@hizb-australia.org |