Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  1 Dhu al-Hijjah 1447 Na: 1447 H / 079
M.  Jumatatu, 18 Mei 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu: Msiruhusu Ardhi Zenu Kuwa Jukwaa la Majeshi ya Wakoloni!
(Imetafsiriwa)

Serikali ya Uingereza imetangaza kupelekwa kwa silaha ya gharama nafuu ya kupambana na droni katika operesheni zake za kijeshi Mashariki ya Kati. Katika taarifa yake, ilisema, “Mfumo mpya sasa umepelekwa katika kumbi za operesheni katika eneo la Mashariki ya Kati.” Pia ilisema kwamba Uingereza “itachangia kwa droni, ndege za kivita, na manuari katika misheni ya kimataifa ili kulinda Mlango-Bahari wa Hormuz.”

Ufaransa pia imetuma meli ya kubeba ndege Charles de Gaulle na kundi la meli zake za kivita Mashariki ya Kati. Yote haya ni pamoja na uwepo wa kijeshi wa Marekani katika ardhi za Waislamu, uwepo wa umbile la Kiyahudi huko Palestina, Lebanon, na Syria, na kambi zake za siri nchini Iraq!

Watawala mafisadi wa Waislamu wamegeuza ardhi zetu kuwa jukwaa la majeshi ya dola za kikoloni za makafiri, kwa badali ya mabwana zao kuwadumisha katika viti vyao vibovu vya utawala. Wanazichana ardhi hizo, wanazuia umoja wake, wanasimama kama kizuizi kisichoshindika dhidi ya utabikishaji wa Uislamu, na kuyageuza majeshi kuwa watumwa na walinzi wao wenyewe na tawala zao za khiyana. Wanazichukulia ardhi hizo kama mali zao binafsi, wakihodhi utajiri na rasilimali zake.

Enyi Majeshi ya Ardhi za Waislamu: Mtakaa kimya hadi lini kuhusu matendo ya watawala hawa Ruwaibidah (wajinga wasio na maana)? Je, nyinyi sio ngome isiyoweza kuingiliwa ya ardhi zenu? Je, si wajibu wenu kulinda ardhi na watu wake? Au je, Aqidah (itikadi) yenu imebadilishwa chini ya kisingizio cha kuwatii watawala, ingawa mnajua kwamba hakuna utiifu kwa kiumbe chochote katika kumuasi Muumba, na kwamba wale mnaowatii leo watawakana Siku ya Kiyama. Kisha, hamtaweza kuwakana katika kisimamo hicho muhimu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt)? Jueni kwamba mnawajibika kwa uhalifu wa watawala katika nchi yenu, na kwamba mnao uwezo wa kuwabadilisha, kwa hivyo fanyeni hivyo kabla hamjajuta wakati mutakuwa mumechelewa sana kujuta!

Enyi Waislamu: Ni wakati wenu wa kujikukuta vumbi la udhalilifu kutoka kwa nafsi zenu, udhalilifu iliosababishwa na watawala wenu Ruwaibidah katika utiifu wao kwa mabwana zao kutoka kwa dola za kikoloni za kikafiri. Ni wakati wenu wa kubadilisha maovu yao. Pamoja na maovu na ukafiri wa wazi unaolindwa na katiba zao zilizotungwa na wanadamu, wameifanya nchi kuwa jukwaa la majeshi ya dola za kikoloni za kikafiri, ambazo haziwatakiini kheri, na ambazo zinapora utajiri wenu na mali ya umma, na kukuzuieni kujitahidi kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu kwa kutabikisha Shariah Yake na kubeba ujumbe Wake kwa watu kama Mtume Mwenyezi Mungu (saw), na Maswahaba zake (ra) na makhalifa baada yake walivyofanya.

Enyi Waislamu: Siku na matukio ya miaka ya hivi karibuni yamewathibitishia kwamba mnao uwezo wa kukabiliana na maadui zenu, na kwamba adui yenu, lau si kwa khiyana ya watawala wenu na njama zao dhidi yenu, hawezi kufanya chochote katika nchi zenu. Kumbukeni kwamba nyinyi ndio Umma bora uliotolewa kwa ajili ya wanadamu kwa sababu ya imani yenu kwa Mwenyezi Mungu na kuamuru kwenu mema na kukataza maovu. Kwa hivyo, harakisheni kwenye mabadiliko ya kweli ambayo Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, inakulinganieni. Fanyeni kazi nayo ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ili kuyafukuza majeshi ya nchi za makafiri kutoka katika ardhi zetu, au kuzifanya kuwa makaburi yao.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-uttahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-uttahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.