Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 29 Ramadan 1447 | Na: 1447 H / 058 |
| M. Jumatano, 18 Machi 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tangazo la Matokeo ya Uchunguzi wa Mwezi Mwandamo wa Shawwal 1447 H na Hongera kwa Idd Al-Fitr Iliyobarikiwa
(Imetafsiriwa)
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa Lillahi Alhamd
Bismillahi Ar-Rahmaan Ar-Rahim, na rehema na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na maswahaba zake, na waliomfuata.
Muslim amepokea katika Sahih yake kupitia kwa Muhammad bin Ziyad ambaye amesema: “Nilimsikia Abu Hurairah (ra) akisema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ، وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ، فَإِنْ غُبِيَ عَلَيْكُمْ فَعُدُّوا ثَلَاثِينَ» “Fungeni kwa kuuona, na fungueni saumu kwa kuuona, na ikiwa umefichika kwenu basi timizeni thalathini.”
Baada ya kuchunguza mwezi mwandamo wa Shawwal katika usiku huu mtukufu, usiku wa Alhamisi, kuonekana kwa mwezi mwandamo kumethibitishwa kwa kuonekana halali kisharia katika baadhi ya nchi za Waislamu. Kwa hivyo, kesho Alhamisi itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal na siku ya kwanza ya Idd al-Fitr iliyobarikiwa.
Kwa mnasaba huu, nawasilisha pongezi zangu na pongezi za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wafanyikazi wake kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, nikimwomba Mwenyezi Mungu ampe ushindi na tamkini ya Uislamu na Waislamu mikononi mwake, ili Umma umpe bayah kama Khalifa wake hivi karibuni, sio baadaye.
Hizb ut Tahrir, pamoja na Amiri wake na wanachama wake kote ulimwenguni, wanamwomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba Idd al-Fitr hii iwe bishara njema kwa Umma wa Kiislamu, na kwamba kurudi kwake juu ya Ummah kuwe huku Mwenyezi Mungu akiupa khilafah, tamkini, na usalama.
Mwaka huu, Idd al-Fitr inakuja huku matukio ya kasi katika ardhi za Waislamu yakichonga ndani ya dhamiri ya Ummah wa Kiislamu mafunzo na tafakari zinazoutikisa na kuondoa dhana potofu na udanganyifu. Imedhihirika kwa Ummah wa Kiislamu, kwa ushahidi wa wazi, kwamba kutafuta msaada wa makafiri (wakoloni) wa Magharibi, au kutumikia maslahi yao ili kupata radhi zake au hata kwa kisingizio cha kuepuka madhara yake, si kitu ila biashara inayopotea ambayo mtendaji wake hafikii chochote ila fedheha katika dunia hii na Akhera.
Hawa hapa watawala wa ardhi za Waislamu ambao wamempa Trump mabilioni na kisha trilioni za dolari kutoka kwa utajiri wa Ummah wa Kiislamu kwa kisingizio cha kununua ulinzi kutoka Amerika, lakini Amerika ikawasha vita katika ardhi zao. Badala yake, Trump anawalazimisha kupigana vita naye ili kufikia maslahi yake.
Vile vile Iran, ambayo ilibaki ikizunguka katika mzunguko wa Amerika kwa miongo kadhaa na kuratibu nayo katika uvamizi wake wa Afghanistan na Iraq, hadi mmoja wa marais wa zamani wa Iran alipotangaza kwamba kama isingekuwa Iran, Amerika ingekuwa imeshindwa kuvamia nchi hizo mbili… Lakini Amerika haitambui fadhila yoyote kwa Iran; badala yake imetangaza vita dhidi yake, hata kumuua kiongozi wake mkuu na inajaribu kupindua serikali yake.
Kinachoendelea katika ardhi za Waislamu kinatufanya tusimame katika mambo mawili:
Jambo la kwanza ni kwamba wito wote wa kujisalimisha kwa Magharibi mkoloni kafiri, ili kuepuka madhara yake au kupata radhi zake, si chochote ila kujiua kisiasa ambako kunasababisha uharibifu na maangamivu kama ambavyo matukio yamethibitisha. Zaidi ya hayo, ni haramu, kinyume na njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kile ambacho Khulafaa’ Rashidun (Makhalifa waongofu) waliendelea nacho, na huleta hasira ya Mwenyezi Mungu (swt) katika ulimwengu huu na Akhera. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاء تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ]
“Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni.” [Al-Mumtahanah:1].
Jambo la pili ni kwamba Waislamu hawapaswi kuhadaiwa na wito wa wakoloni makafiri wa Magharibi na vibaraka wao kwamba Waislamu hawawezi kuregesha mamlaka yao kutoka humo. Uwezo ambao Magharibi inao hauzidi ule unaoonekana na macho. Hii hapa Amerika, ambayo jeshi lake limepandishwa cheo duniani kama nguvu kubwa zaidi ya kijeshi duniani, lakini imeshindwa kufikia kile ilichodanganya dunia nacho, kwamba vita vyake na Iran vingekuwa vita vya haraka kama vile ilivyofanya nchini Venezuela. Vita vimeendelea na vimekuwa vigumu, na hali imekuwa ngumu kwa Trump na mabwana zake, kwa hivyo wakaanza kutoa uongo baada ya uongo kuhusu mafanikio yao katika kuondoa uwezo wa kijeshi wa Iran huku wakitafuta njia ya kutoka katika hali yao ngumu.
Kwa hivyo, kwa mnasaba huu wenye baraka, tunaulingania Ummah wa Kiislamu kuamsha hisia za furaha katika Idd yake licha ya adui yake. Hebu na uifanye Idd hii ya Fitr kuwa hali ya matumaini katika ushindi na tamkini. Hebu na ukumbuke kwamba Khilafah ni mfumo wa kisiasa ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliuongoza, na ni mfumo wa kisiasa uliotekelezwa na Maswahaba (Mwenyezi Mungu awe radhi nao), ambao ulidhamini heshima ya Umma wa Kiislamu katika historia yake yote, na haukuwa na heshima isipokuwa chini yake. Umma lazima ujishughulishe na kazi ya kuuregesha sasa na kuufanya kuwa ndio lengo lake kuu.
Wanachama wa Hizb ut Tahrir wamejiandaa kuregesha faradhi hii kubwa kwa thaqafa ya Kiislamu na ufahamu wa kisiasa. Wako miongoni mwenu na pamoja nanyi, wakinyoosha mikono yao kwenu, wakitumai kwamba Mwenyezi Mungu atatupa sisi na nyinyi ushindi na tamkini. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ametupa bishara yake njema kuhusu yatakayokuja baada ya utawala huu dhalimu katika Hadith iliyopokelewa na Hudhayfah, ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ». “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza.”
Idd Mubarak
Wassalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu
Usiku wa kuamkia Alhamisi, siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal, kwa mwaka wa Hijri wa 1447, sawia na 19 Machi 2026 M.
Mhandisi Salah Eddin Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-uttahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-uttahrir.info |