Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hatimaye, Dhalimu Trump Anahitimisha Ziara yake katika Kanda hii
(Imetafsiriwa)

Trump alianza ziara yake nchini Saudi Arabia mnamo Mei 13, 2025, ikifuatiwa na Qatar mnamo Mei 14, 2025, akihitimisha safari yake nchini Imarati mnamo Mei 15, 2025, na kuhitimisha ziara yake mnamo Mei 16, 2025. Kisha aliandamanisha ziara hii kwa udanganyifu wake kwamba hatazuru umbile la Kiyahudi, kuwakejeli wajinga wanaodai kuwa uungaji mkono wa Trump kwa umbile la Kiyahudi umetikiswa! Hii ni licha ya ukweli kwamba umbile la Kiyahudi lilipanua mashambulizi yake kwenye Ukanda wa Gaza baada ya Trump kuondoka katika nchi hizo tatu. Ni hakika kwamba umbile la Kiyahudi haliwezi kuanza au kupanua uvamizi wake dhidi ya Ukanda wa Gaza bila idhini kamili ya Marekani, hasa wakati wa utawala wa Trump! Trump hakuishia hapo, bali aliweka wazi kwao, hadharani na si kwa siri, kuhusu dili zake za ardhi na majumba katika Ukanda wa Gaza: Trump alieleza kutoka Qatar: “Nina fahamu kuhusu Gaza ambazo nadhani ni nzuri sana...” na nadhani ni eneo muhimu sana kwa mtazamo wa dili za majumba...”. Trump kwa mara nyengine alipendekeza kuwahamisha Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza na kuwapeleka katika nchi nyinginezo, ambazo alisema “ziko tayari kuwapokea” (BBC, Alhamisi, 15/5/2025). Pasi na shaka yoyote, uovu wanaouamua! Na hivi ndivyo walivyompokea:

1- Trump alifika jijini Riyadh na kukaribishwa kwa furaha, kana kwamba ameshuka kutoka mbinguni kama mwokozi na mkombozi, sio adui wa Uislamu na Waislamu. Aliitambua Al-Qudsi kuwa mji mkuu la Mayahudi, akahamisha ubalozi wake huko, na kuiunganisha Milima ya Golan kwa umbile la Kiyahudi. Walimkaribisha kwa uchangamfu, ingawa alitangaza katikati yao kwamba alitaka kuzurura kwa uhuru katika Ukanda wa Gaza, kuununua na kuuuza, na kuwahamisha watu wake. Walimkaribisha kwa furaha, ingawa alisema mbele yao wakati wa muhula wake wa kwanza: “Rais wa Marekani Donald Trump aliendelea kuitaka Saudi Arabia ilipie ulinzi wa Marekani kwa Ufalme huo.” Kwa mara ya tano katika muda usiozidi wiki mbili, Trump alimtaka Mfalme wa Saudi Salman bin Abdulaziz alipie ulinzi, akisema kwamba Saudi Arabia haingekuwepo bila ulinzi wa Marekani.” (Al Jazeera, Oct. 11, 2018). Kisha, kabla hajaondoka, wanampa pesa za Waislamu: “Ikulu ya White House ilisema kwamba Rais Trump anadhamini ahadi ya kihistoria kwa Saudi Arabia kuwekeza dolari bilioni 600 nchini Marekani. Aliongeza kuwa Marekani na Saudi Arabia zilitia saini makubaliano makubwa zaidi ya mauzo ya ulinzi katika historia, yenye thamani ya takriban dolari bilioni 142.” (Al Jazeera, 13/5/2025).

Hakuishia katika kupora pesa za Waislamu, bali alikwenda mbali zaidi kwa kuhalalisha mahusiano na Mayahudi: “Rais wa Marekani, Donald Trump alisema mnamo Jumanne kwamba Saudi Arabia hivi karibuni itajiunga na Makubaliano ya Abraham... Aliongeza kuwa ana matumaini makubwa kwamba Saudi Arabia hivi karibuni itatia saini makubaliano ya kuhalalisha mahusiano na 'Israel'.” (Sky News Arabia, 13/5/2025.) Kisha, “Trump alikutana na rais wa mpito Ahmed al-Sharaa jijini Riyadh kabla ya kuelekea Qatar katika siku ya pili ya ziara yake katika kanda hiyo. Rais wa Uturuki Erdogan alihudhuria mkutano huo kupitia mtandao...” (BBC, 14/5/2025). Gazeti la Uingereza la, ‘The Times’ lilifichua undani wa hali ya Ahmed al-Sharaa: The Times liliongeza “Sharaa ameongeza hata uwezekano wa kuwepo Mnara wa Trump jijini Damascus, mji mkuu wa Syria, kama sehemu ya mazungumzo yake kwa rais wa Marekani kupitia ... jaribio la kumshawishi rais wa Marekani, kupitia wasuluhishi wanaoaminika kujumuisha watu mashuhuri nchini Saudi Arabia na Uturuki”... Gazeti la Times liliripoti kuwa al-Sharaa huenda akajitolea kuanza mazungumzo ya kujiunga na Mkataba wa Abraham, kwa mujibu wa kile gazeti la Uingereza lilijua kutoka kwa vyanzo vya usalama... (BBC, 13/5/2025). Kama inavyoweza kueleweka kutokana na hili, Mohammad Bin Salman na rais wa Uturuki walikuwa "wadhamini" wa hili!

2- Kisha anasafiri hadi Qatar, ambako anakaribishwa kama rafiki, sio adui. Yeye ndiye aliyewalazimisha kuwa kitovu cha kujadiliana na Mayahudi, ili kuwapa kupiti njia ya mazungumzo yale wasiyoweza kuyapata katika vita na kundi dogo la waumini, wasio na vifaa vya kutosha, na wasio thabiti. Aliwalazimisha kuwa kituo cha kujadiliana na Mayahudi kana kwamba Qatar haiegemei upande wowote, bali wao wako karibu zaidi na Mayahudi. Kisha wanamkaribisha kama rafiki na kipenzi, na kuzuru kambi yake iliyo miongoni mwao, wakishindwa kuikataa kambi yake, licha ya kuwa ndicho kitovu cha vita vya Marekani dhidi ya Waislamu popote walipo. Trump anaiambia kambi yake, mbele ya Qatar: “Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza mnamo Alhamisi kwamba Qatar itawekeza dolari bilioni 10 katika Kambi ya Anga ya Al Udeid, kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani katika Mashariki ya Kati...” (Sky News Arabia, 15/5/2025). Trump alikuwa akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara yake nchini Qatar.

3- Kisha Trump anasafiri hadi UAE, kituo chake cha tatu na cha mwisho katika ziara yake ya Ghuba ... na kuona huko asichokiona mahali pengine popote! Wanafunga msikiti ili kumkaribisha; wanafunga msikiti ili kumuenzi! “Trump aliwaambia waandishi wa habari ndani ya msikiti ... “Kwa mara ya kwanza wanaufunga. Ni kwa ajili ya heshima ya Marekani, nadhani. Bora kuliko kwa heshima yangu. Tuisifieni nchi hiyo. Hiyo ni pongezi kubwa.” Na Bin Zayed akamtunuku Trump nishani ya Zayed - heshima kubwa zaidi ambayo UAE inawapa wakuu wa nchi, wafalme, na marais. Kisha uwekezaji wa UAE kufikia dolari trilioni 1.4: Rais wa UAE alitangaza, wakati wa kumpokea mwenzake wa Marekani katika Qasr Al Watan jijini Abu Dhabi, kwamba nchi yake itawekeza dolari trilioni 1.4 katika miaka kumi ijayo. (BBC, 15/5/2025). Kisha Trump anajigamba juu ya mali alizopora wakati wa ziara yake kutoka kwa Waislamu kwa kuwasaliti watawala wao, akiwaambia: "Hii ni ziara ya rekodi. Hakutawahi kuwa na ziara ambayo itakayokusanya - inaweza kuwa jumla ya $ 3.5, $ 4 trilioni. Katika siku hizi nne au tano tu.” (BBC, Mei 15, 2025). Kisha Trump aliondoka eneo hilo kwenye zulia la buluu baada ya kuvuna zawadi zake” ...Trump alitoka hadi kwenye uwanja wa ndege wa Abu Dhabi akifuatana na Rais wa UAE Sheikh Mohammed bin Zayed, na viongozi hao wawili wakafanya mazungumzo ya kando kwenye zulia la buluu.” (CNN, 16/5/2025)

4- Hivi ndivyo watawala wa nchi za Kiislamu wanavyompokea bila aibu yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, au waumini! Na ilhali, "anafanya biashara nao" na kwa pesa za Waislamu, akipora pesa za Waislamu ambazo watawala hao hawamiliki: “Nchini Qatar, Trump alisema kwamba ziara yake ya Ghuba inaweza kutoa mikataba yenye thamani ya hadi dolari trilioni nne, wakati wa mkutano na wafanyibiashara jijini Doha. Akaongeza, "Hii ni ziara ya rekodi. Hakujawahi kuwa na ziara ambayo itaongeza - inaweza kuwa jumla ya $ 3.5, $ 4 trilioni. Katika siku hizi nne au tano tu." (BBC, 15/5/2025).

5- Ni dhambi kubwa kuwa watu hawa ni watawala wa ardhi za Kiislamu, wakaigeuza nchi kuwa uwanja wa michezo wa Trump na mfano wake, ambapo wanazurura ovyo. Ni dhambi kubwa kwamba watu hawa ni watawala wa ardhi za Kiislamu, wakiwapigia makofi Makafiri, maadui wa Uislamu na Waislamu, kugeuza khiyana kuwa uaminifu, kusema uwongo katika ukweli, na kudhibiti mambo ya umma kwa njia ya uovu na uharibifu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema kweli katika hadith yake iliyopokelewa na Ahmad kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«إِنَّهَا سَتَأْتِي عَلَى النَّاسِ سِنُونَ خَدَّاعَةٌ، يُصَدَّقُ فِيهَا الْكَاذِبُ وَيُكَذَّبُ فِيهَا الصَّادِقُ، وَيُؤْتَمَنُ فِيهَا الْخَائِنُ وَيُخَوَّنُ فِيهَا الْأَمِينُ، وَيَنْطِقُ فِيهَا الرُّوَيْبِضَةُ. قِيلَ: وَمَا الرُّوَيْبِضَةُ؟ قَالَ: السَّفِيهُ يَتَكَلَّمُ فِي أَمْرِ الْعَامَّةِ»

Hakika itawajia watu miaka ya udanganyifu, ambapo muongo ataaminiwa, na mkweli atakadhibishwa, msaliti ataaminiwa na waaminifu atasalitiwa, na wajinga watakuwa wazungumzaji." Iliulizwa, "Ni nani wajinga?" Akasema, "Safihi ambaye anazungumzia mambo yanayohusu umma.”

6-  Enyi Waislamu:

[وَلَا تَيْأَسُوا مِنْ رَوْحِ اللهِ إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِنْ رَوْحِ اللهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ]

“Wala msikate tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri.” [Yusuf 12:87]. Haijalishi Trump ana kiburi kiasi gani au kiburi chake kina shinda kiasi gani, hatima yake itafikia mwisho, kama ilivyotokea kwa watu wake waliomtangulia. Mtawala huyu dhalimu aliyezingirwa na udhalimu wake amesahau, au kujifanya kusahau, yaliyowapata wafuasi wake kabla yake. Wafalme wa Kifursi na wafalme wa Kirumi walimtangulia katika udhalimu wao baada ya kuasi. Kisha Mwenyezi Mungu akawanusuru kutoka pale ambapo hawakutarajia, kwa jihad, ufunguzi wa ardhi, na kuwaangaza kwa nuru ya Uislamu. Hata wawe waovu vipi watawala wa Waislamu, wataangamia, Mwenyezi Mungu Akitaka. Ardhi za Waislamu ni safi, na hakuna Makafiri wakoloni watakaokaa humo wanaotaka kuzinajisi.

7- Enyi Waislamu: Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, imehakikishiwa kwamba utawala huu dhalimu tunaoishi chini yake utakwisha, na Khilafah Rashida itarejea tena, Mwenyezi Mungu akipenda. Imepokewa kutoka kwa Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Hudhayfah, ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema: «...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ» Kisha utakuwa ni utawala wa dhulma, na utakuwa kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha atauondoa atakapokuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya utume, kisha akanyamaza.” Hata hivyo, Sheria za Mwenyezi Mungu zinaagiza kuwa hatateremsha Malaika kutoka mbinguni ili wasimamishe Khilafah kupigana na adui yetu huku tukiwa tumepakata mikono, bali anawateremsha Malaika wake wawe wasaidizi na bishara njema ya ushindi wake, kwa watu waliomuamini Mola wao na akawazidishia uongofu, wanajeshi wa Kiislamu, wenye subira vitani, wanaomuogopa Imam wao na kupigana nyuma yake na dhidi ya maadui zao na kurejesha Khilafah yao na hapo ndipo watakuwa na bishara njema.

[نَصْرٌ مِنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ]

ushindi ulio karibu! Na wabashirie Waumini! [As-Saf 61:13]

H. 20 Dhu al-Qi'dah 1446
M. : Jumapili, 18 Mei 2025

Hizb-ut-Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.