Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mwangwi wa Himaya: Uharamia wa Marekani Pwani ya Venezuela

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 10 Disemba 2025, Marekani ilimkamata nahodha wa meli ya mafuta kutoka pwani ya Venezuela, ikipanda meli hiyo na kuelekeza shehena yake ya takriban mapipa milioni 1.8 ya mafuta ghafi ya Venezuela hadi Marekani chini ya kibali cha vikwazo vya Marekani ambacho kilikuwa kinakaribia kuisha. Maafisa wa Marekani walidai hatua hii ya utekelezaji ililenga kuadhibu ukiukaji wa vikwazo vya muda mrefu vinavyohusiana na madai ya usafirishaji haramu wa mafuta. Serikali za Venezuela na Cuba zililaani hatua hiyo kama “wizi wa waziwazi” na “uharamia,” huku Cuba ikiuita “ugaidi wa baharini” ikiathiri mahitaji yake ya nishati. Usumbufu huo umeacha zaidi ya mapipa milioni 11 ya mafuta ya Venezuela yamekwama baharini, huku meli za mafuta na wafanyibiashara wakitathmini upya hatari za kubeba mafuta ghafi ya Venezuela, na kulazimisha punguzo kubwa na mazungumzo ya mikataba na wanunuzi muhimu kama vile China.

Maoni:

Kukamatwa kwa Nahodha na Marekani — ambako kulihusisha Walinzi wa Pwani wa Marekani na vikosi vya kijeshi kuchukua udhibiti wa meli ya mizigo ya mafuta ya Venezuela katika bahari za kimataifa — si zoezi la kutekeleza sheria; linaonyesha uthibitisho uliopigiwa hesabu wa nguvu ya upande mmoja juu ya uhai wa kiuchumi wa dola huru, nje unaohalalishwa kwa vikwazo lakini ukifanya kazi kivitendo kama utaratibu wa ushawishi wa siasa za kijiografia. Kihistoria, mahusiano kati ya Washington na Caracas yameundwa na vipindi vya ushirikiano na udhibiti unaoendeshwa na maslahi ya mafuta. Tangu mwanzoni mwa karne ya 20, maslahi ya Marekani katika mafuta ya Venezuela yameathiri sera, kuanzia kuunga mkono udhibiti wa makampuni ya mafuta ya Marekani hadi kukabiliana na utaifishaji na migogoro katika sekta ya mafuta ya Venezuela. Nyaraka za sera za Marekani zinaonyesha kwamba kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya mafuta kwa muda mrefu imekuwa lengo la kimkakati linalounga mkono sera ya kigeni ya Marekani kwa Venezuela.

Kukamatwa kwa Nahodha mwaka 2025 kufuatia miaka ya shinikizo linaloongezeka ambalo linajumuisha vikwazo vikubwa vilivyowekwa tangu 2019 kwa kampuni ya mafuta ya serikali ya Venezuela PDVSA na washirika wake wa biashara. Vikwazo hivi vimezuia mara kwa mara uwezo wa Caracas kujihusisha na masoko ya mafuta duniani, hata wakati msamaha usio rasmi ulipotolewa ili kudumisha mtiririko mdogo. Athari jumla ya vikwazo tayari imepunguza uwezo wa uzalishaji wa mafuta wa Venezuela na msingi wa mapato; kukamatwa kwa Nahodha kunaongeza madhara haya kwa kukatiza usafirishaji nje na kutuliza kabisa safari za meli za mafuta. Wafanyibiashara wamejibu kwa kusimamisha usafirishaji na kudai punguzo kubwa, na hivyo kuiadhibu Venezuela katika masoko ghafi ya kimataifa.

Huku utawala wa Trump ukielezea hatua hizi kama zinazolenga “mitandao haramu” au sehemu ya mkakati wa kupambana na dawa za kulevya, muundo mpana wa msimamo wa kijeshi na kuzuia rasilimali unaangazia kwamba lengo hilo linapanuka zaidi ya kuwatenga wahusika wa uhalifu. Katika miezi ya hivi karibuni, Marekani imeongeza kwa kiasi kikubwa uwepo wake wa kijeshi Kusini mwa Caribbean na kufanya mashambulizi kwenye meli inazodai zinahusishwa na biashara ya dawa za kulevya - vitendo ambavyo vimeibua wasiwasi hata miongoni mwa wasomi wa sheria kuhusu maumbile yake ya nje ya sheria na uwezekano wa ukiukaji wa desturi za kimataifa. Operesheni hizi zinasadifiana na majadiliano mapana ndani ya duara za sera za Marekani kuhusu kupindua au angalau kudhoofisha udhibiti wa serikali ya Maduro wa madaraka.

Caracas inadhibiti mojawapo ya akiba kubwa zaidi ya mafuta ghafi iliyothibitishwa duniani, na muegemeo wake wa kisiasa — hasa ushirikiano wake na mataifa kama China, Urusi, na Cuba — unatishia nyanja ya ushawishi wa Washington katika kile inachokiona kama uwanja wake wa nyuma. Kwa hivyo, uharamia na mauaji ya Marekani huko Caribbean husababisha kusita kwa waendeshaji wa meli za mafuta za kimataifa kupakia mafuta ghafi ya Venezuela — wakiogopa kukamatwa zaidi, jambo ambalo linaweka mamlaka ya nevi ya Marekani juu ya haki za kibiashara za wazalishaji huru ili kuunda upya miundo ya biashara kwa faida ya Washington.

Kwa pamoja, mambo haya yanayojiri yanaonyesha kwamba nia ya msingi ya kukamatwa kwa Nahodha huyo na hatua zinazohusiana sio tu kuhusu kutekeleza vikwazo. Ni sehemu ya kampeni ya kimkakati inayolenga kulazimisha makubaliano ya kiuchumi na kisiasa kwa kutumia udhibiti wa moja kwa moja juu ya mauzo ya nje ya mafuta ya Venezuela, na hivyo kudhoofisha uhuru wa serikali ya Maduro. Kwa kweli, Washington inatumia unyimaji wa kiuchumi na shinikizo la kijeshi kama vyombo vya ushawishi, ukumbusho wa mabadiliko ya kihistoria ambapo dola kubwa zilitumia utegemezi wa rasilimali kuunda siasa za ndani za dola dhaifu.

Kivitendo, hii ina maana kwamba watu wa Venezuela — ambao riziki zao na miundombinu ya kitaifa imeunganishwa sana na mapato ya mafuta — wanabeba matokeo ya mzozo ambapo utajiri wa asili wa nchi yao unakuwa kikwazo cha majadiliano katika ujanja wa siasa za kijiografia. Mbali na kulinda uhuru au sheria za kimataifa, kukamatwa kwa Nahodha kunaimarisha mfumo wa dunia ambapo dola zenye nguvu hutafsiri upya mifumo ya kisheria ili kuhalalisha vitendo vinavyotumikia maslahi yao ya kimkakati huku zikidhoofisha haki za ubwana za wengine. Ubaguzi kama huo wa upande mmoja hudhoofisha masoko ya kikanda, huzidisha ugumu wa kiuchumi, na humomonyoa desturi zinazopaswa kusimamia kuishi kwa amani miongoni mwa mataifa, lakini desturi pekee ambayo Marekani inathamini ni kuhalalisha maslahi yake kama yanayotawala na kando na maslahi mengine yoyote.

Tunachokiona kuhusu uharamia wa Marekani katika Caribbean ni mwendelezo mwingine tu wa mkono wake wenye damu juu ya watu wa dunia ambao inayoiona kama shamba lake la kibinafsi la kujinufaisha mwenyewe inavyotaka bila kujali gharama yoyote ile kwa wanadamu.

[وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Quran, 14:42]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.