Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mpango wa Trump wa Gaza ni Mpango Muovu wa Usaliti Unaolenga Kuangamiza Kadhia ya Palestina

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa Waziri Mkuu wa “Israel” Benjamin Netanyahu amekubali mpango wenye vipengee 20 ambao ungemaliza vita katika Ukanda wa Gaza. Trump na Netanyahu walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya mkutano wao jijini Washington. Trump alisema kuwa amani ya Gaza ilikuwa karibu sana kupatikana na kumshukuru Netanyahu kwa kuidhinisha mpango huo (DW Turkish 29.09.2025).

Maoni:

Huku vita mjini Gaza vikiingia mwaka wake wa tatu, Trump, mfuasi mkubwa wa mauaji haya ya halaiki, alitangaza kile kinachoitwa mpango wa amani kuhusu Gaza mnamo Septemba 29. Mpango huo ulitangazwa kwa mara ya kwanza kama vipengee 21; baadaye ulirekebishwa kulingana na maslahi ya Marekani na umbile la Kiyahudi na kupunguzwa hadi vipengee 20.

Kwa yeyote atakayeisoma ataelewa kwa urahisi kwamba, mpango wa Trump wa Gaza ni mpango muovu wa usaliti unaolenga kufilisisha kikamilifu kadhia ya Palestina kwa kuupokonya silaha upinzani, kwa sababu kila kifungu cha mpango huo kiko na kusalim amri bila ya masharti kwa mujahidina na wananchi wa Palestina.

Kifungu cha kwanza kinataka Gaza “isafishwe kutokana na itikadi kali na ugaidi”. Kwa maana nyengine, Waislamu mjini Gaza ambao wanalinda ardhi yao na maadili matakatifu dhidi ya mvamizi wanaitwa “magaidi.” Hakuna maregeleo hata moja ya uhalifu wa gaidi halisi, Israel muuaji wa watoto. Kifungu cha nne kinatoa masharti ya kuachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas. Kwa upande wake, inasemekana kuwa wafungwa 1,700 wa Kipalestina wataachiliwa huru. Lakini hakuna dhamana katika suala hili ima; kwa sababu uwepo wa Mayahudi unaweza kuwakamata wafungwa ambao imewaachilia huru wakati wowote inapotaka.

Vifungu vikuu ambavyo huunda kiini cha mpango huo ni kifungu cha sita na kumi na tatu. Kwa mujibu wa vifungu hivi viwili, mujahidina wa Qassam watasalimisha silaha zao kwa adui na mahandaki na vituo vya kutengeneza silaha huko Gaza vitaharibiwa. Kwa hivyo, watu wa Gaza wataachwa kabisa chini ya huruma ya umbile la Kiyahudi. Ikiwa haya yatatokea, misaada ya kibinadamu itaingia Gaza na shughuli za ujenzi na maendeleo zitaanza. Hata hivyo, msaada huu hautatolewa kulingana na mahitaji ya kibinadamu; itatolewa kwa kiasi kidogo, kidogo kidogo, na tena kwa namna ya polepole. Zaidi ya hayo, sio kwa Gaza nzima, lakini kwa maeneo “yasiyo na ugaidi”, kama wanavyoyaita. Wakati huo huo, hakuna uhakika kwamba uvamizi huo utaisha. Suala hilo liliachwa wazi kwa kusema “ikiwa itahakikishwa kuwa ugaidi umekwisha” huko Gaza. Hii inamaanisha kuwa uvamizi kamwe hautakwisha!

Netanyahu alitoa mukhtasari wa kile mpango huo ulimaanisha baada ya mkutano wake na Trump: “Badala ya Hamas kututenga, tumegeuza meza na kuwatenga Hamas.” “Sasa dunia nzima, ikiwa ni pamoja na ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, inawashinikiza Hamas kukubali masharti tuliyoweka.” “Kuwaachilia mateka wetu wote, walio hai na waliofariki, huku IDF ikibakia katika sehemu kubwa ya Ukanda.” Ndio, kama Trump na Netanyahu walivyosema mara kwa mara, madhumuni ya mpango huo ni kuichukua Gaza na kuendeleza ukaliaji kimabavu na ukatili, na bila gharama yoyote katika Gaza isiyo na silaha na upinzani.

Jambo la kusikitisha zaidi ni usaliti wa wale wanaojiita viongozi wa Waislamu ambao Netanyahu alisema, “wanawashinikiza Hamas kukubali masharti tuliyoweka.” Viongozi hawa wanahusika kwa Gaza kutelekezwa na makafiri kuwa na kiburi na kutojali. Hawamwogopi Mwenyezi Mungu wala hawaoni haya kwa Ummah. Hata Trump awatusi kiasi gani, hawamwachi; wanashindana kukutana naye kwa dakika 5 na kupata uhalali kutoka kwake. Viongozi hawa walijitokeza kwa mara ya kwanza kwenye meza ya Trump jijini New York, na kisha mara moja wakaeleza kuridhika kwao wakati Trump alipotangaza mpango wake wa uhaini.

Sasa viongozi hawa wanajiandaa kwa usaliti mkubwa ambao utapita kama doa jeusi kwenye historia kwa kisingizio cha kusimamisha umwagaji damu huko Gaza na amani ya kikanda. Uturuki, Qatar, Jordan, Pakistan, Saudi Arabia na Indonesia zote zimekuwa zikifanya kazi kwa bidii kuwafanya mujahidina waweke chini silaha zao. Kwa sababu walitoa ahadi ya maandishi kwa Trump juu ya suala hili. Na haikufungika tu kwa hili; wakati huo huo, baadhi ya nchi hizi zitatuma majeshi yao huko Gaza. Sio kuwalinda watu wa Gaza, bali kuwalinda askari magaidi wa uwepo wa Mayahudi kutoka kwa Waislamu wa Palestina. Zaidi ya hayo, nchi hizi zinataka kuijenga upya Gaza, ambayo Mayahudi wameigeuza kuwa magofu, kwa kubeba gharama na mwishowe, wanataka kuiwasilisha Gaza kama tuzo kwa Trump kafiri kwa kutoa mali ya ummah. Badali yake, watapata tu “pongezi” kutoka kwa Trump, na kisha watasonga kwa haraka kuhalalisha mahusiano na umbile la Kizayuni. Hakika udhalilifu mkubwa namna hii haujawahi kuonekana katika historia ya umma wa Kiislamu.

Hivyo basi, ni wajibu wa kila Muislamu anayeunga mkono kadhia ya Palestina kukataa mpango huu wa khiyana na watetezi wake—ambapo inamaanisha kujiua kisiasa, ambako kunachukuliwa kuwa ni dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt)—kuwapinga, na kufanya kazi ya kuzima mpango huo.

Kama Shahidi Yahya Sinwar alivyosema: “Mji huu (Jerusalem-Gaza) utawaanika watu wote wenye kuhalalisha mahusiano, kuwafedhehesha washirika wote, na kufichua sura ya kweli ya wale wanaokata tamaa na kulegeza msimamo.”

Mpaka nusra ya Mwenyezi Mungu (swt) iwafikie wenye subira na kumtegemea Yeye.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Mohammad Amin Yıldırım

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.