Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tamasha la OIC Lahitimisha kwamba Qatar na Dola za Kiarabu Zisalie Waaminifu kwa Kuwa Kiatu Kilicho Chakaa cha Amerika Huku Zikibweka Vikali Mawinguni

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kufuatia shambulizi la kombora la umbile la Kizayuni dhidi ya wanachama wa Hamas nchini Qatar, taarifa ya mwisho ya mkutano wa dharura wa kilele wa Waarabu-Waislamu (OIC na Ligi ya Waarabu) uliofanyika jijini Doha mnamo 15 Septemba 2025, “unashutumu vikali uvamizi wa Israel dhidi ya Qatar, na kuutaja kuwa ni kama pigo kwa matarajio yoyote ya amani katika eneo hilo. Tangazo hilo zilizisihi nchi wanachama kuzingatia upya mafungamano yao ya kidiplomasia na kiuchumi na Israel na kufuata hatua za kisheria dhidi yake.”

Maoni:

Rasimu ya taarifa ya awali ilionya kwamba hatua hizi zinahatarisha “kila kitu ambacho kimefikiwa katika njia ya kuhalalisha mafungamano na ‘Israeli’, ikiwemo makubaliano ya sasa na ya mustakbali.” OIC na Ligi ya Nchi za Kiarabu zinaendelea na shutma zao na maonyo yao kama ambavyo zimekuwa zikifanya kwa miaka na miongo kadhaa na ilhali ‘hali ni kama kawaida’ kwa wanachama wa Ligi ya Nchi za Kiarabu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Imarati Sheikh Abdullah bin Zayed alikutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu pembezoni mwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, kulingana na shirika la habari la serikali la Imarati mnamo tarehe 27 Septemba ambapo alisisitiza haja ya haraka ya kumaliza vita vya Gaza huku akisisitiza “dhamira isiyoyumbayumba ya Imarati ya kuunga mkono mipango yote inayolenga kufikia amani pana kwa msingi wa suluhisho la dola mbili, kwa namna ambayo itatimiza matarajio ya watu wa Palestina na Israel.” Wakati kauli za viongozi wa Kiarabu na utawala wa Marekani zikizingatiwa bega kwa bega hakuna tofauti inayoweza kuonekana isipokuwa katika matamshi. Utawala wa Marekani unajivunia mapenzi yake kwa Mayahudi na uungaji mkono wake wa milele kwa umbile la Kizayuni, huku viongozi wa Kiarabu wakilaani jinai za umbile hilo la Kizayuni. Hata hivyo, bwana na vibaraka kwenye kamba yake wanakubaliana juu ya uoanishwaji kamili wa umbile la Kizayuni ndani ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu na wanayaona mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina kama kikwazo kwa lengo lao la pamoja.

Hata kwenye suluhisho la dola mbili, dola ya Palestina na ya Kiyahudi zikiishi bega kwa bega, hakuna tofauti. Trump hata aliondoa baadhi ya shinikizo la ndani kwa Netanyahu kutoka ndani ya serikali yake kwa kusema hadharani kwamba uunganishwaji wa Ukingo wa Magharibi “hautatokea” iwe kwa kuwepo au bila ya kuwepo dola ya Palestina, Ligi ya Nchi za Kiarabu itabaki kuwa puto tupu lililojaa hewa ya moto inayodumisha udhibiti wa Marekani juu ya mamia ya mamilioni ya watu wa Mashariki ya Kati ili wale wanaojiita viongozi wa nchi wanachama wake waweze kudumisha viti vyao vya utawala, wanavyokalia juu yake kama vikaragosi tu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.