Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uongozi wa Kiislamu Unapokosekana, Ukandamizaji Hutawala

(Imetafsiriwa)

Habari:

Marekani Yapeleka Manuari Venezuela; Maduro Awakusanya Wanamgambo Milioni 4.5 (latinamericareports.com/)

Maoni:

Marekani kwa mara nyengine tena imefichua hali yake ya kiuadui ya sera yake ya kibeberu ya mambo ya nje kwa kutuma manuari tatu kuelekea pwani ya Venezuela. Washington inahalalisha hatua hiyo kupitia tuhuma za muda mrefu kwamba Venezuela inashiriki katika ulanguzi wa madawa ya kulevya-shtaka ambalo Caracas inakataa vikali kama lisilo na msingi na linalochochewa kisiasa.

Kwa kujibu, serikali ya Venezuela ililaani ujanja huo kama kitendo cha kutapatapa: “Jamhuri ya Bolivar ya Venezuela inaona kwa uwazi kabisa hali ya kutapatapa ya utawala wa Marekani, ambayo inaamua kutumia vitisho na kashfa dhidi ya nchi yetu. Tuhuma za Washington kwamba Venezuela inahusika katika ulanguzi wa madawa ya kulevya zinaonyesha ukosefu wao wa uaminifu na kufeli kwa sera zake katika eneo hili.”

Rais Nicolás Maduro alisisitiza tena ubwana wa Venezuela licha ya vitisho vya kigeni, na kutangaza: "Bahari zetu, anga zetu, na ardhi zetu zinahamiwa na sisi, zimekombolewa na sisi, zinalindwa na kupigwa doria na sisi. Hakuna himaya yoyote itakayokuja kugusa ardhi takatifu ya Venezuela, wala kusubutu kugusa ardhi takatifu ya Amerika ya Kusini - hakuna himaya yoyote dunia hii.”

Kwa miongo kadhaa, Marekani imekuwa ikitegemea nguvu za kijeshi kutekeleza udhibiti wake wa kisiasa na kiuchumi kote Amerika ya Kusini, Mashariki ya Kati na kwengineko. Mataifa yanayojaribu kutangaza uhuru yanaadhibiwa kwa vikwazo, kampeni za propaganda, au vitisho wazi vya kijeshi. Masaibu ya sasa ya Venezuela ni mfano wa mpya zaidi wa mfumo wa dunia unaodumishwa sio kupitia uadilifu, bali kupitia nguvu na unyonyaji.

Hata hivyo, huku Caracas ikipinga, inasalia imenaswa katika mfumo wa kimataifa unaodhibitiwa na taasisi za kifedha na kisiasa za Magharibi. Uasi ndani ya mfumo huu hauwezi kupata uhuru wa kweli; unarefusha tu utiishwaji chini ya utaratibu ule ule usio wa dhulma.

Wanachohitaji wanadamu ni ruwaza badali—ambayo inavuka kufeli kwa siasa za Magharibi. Ubepari, uliojengwa juu ya unyonyaji na umwagaji damu, hautoi uadilifu wa kudumu. Uislamu, kinyume chake, umekita mizizi katika haki, huruma, na uadilifu, ukisimama katika historia yote pamoja na wanyonge dhidi ya madhalimu wao.

Kile dunia inachohitaji leo ni uongozi unaojikita katika kanuni hizi. Khilafah sio tu mfumo badali; ni muundo pekee wenye uwezo wa kuvunja duara la udhibiti wa kibeberu na kusimamisha mfumo adilifu wa ulimwengu.

[وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُواْ شُهَدَاء عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا]

“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu.” [Qur’an 2:143]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa ut Tahrir in Amerika

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.