Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wanachama wa Hizb ut Tahrir huko Abbasiya Watangaza: Tibueni Mpango wa Amerika wa Kutenganisha Darfur
(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al-Rayah - Toleo 564 - 10/09/2025 M

Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan kutibua mpango wa kuichana Sudan kwa kutenganisha eneo la Darfur, na kwa kuzingatia kwamba umoja wa Ummah ni suala nyeti, ambalo ni lazima hatua za uhai au kifo zichukuliwe, Mashababu (wanachama) wa Hizb ut Tahrir walifanya mkutano mnamo Ijumaa, 6 Rabi’ al-Awwal 1447 H, sawia 29 Agosti 2025 M, baada ya swala ya Ijumaa, katika Msikiti wa Sheikh Yahya wa Kuhifadhi Qur'an. Walitoa wito wa dhati kwa Waislamu wa makundi yote, wakiwemo wanasiasa, wanahabari, maulamaa, maafisa na wanajeshi, na wengineo, wakiwataka watimize wajibu wao wa Shariah wa kuzuia kujitenga kwa Darfur.

Wito huo ulisomwa na Ustadh Abdul Rahim Abdullah, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, katikati ya umati mkubwa wa waumini. Waliosimama kuliani kwake na kushotoni walikuwa baadhi ya Mashababu wa Hizb wakiwa wakibeba mabango ya kutoa wito wa kupinga kujitenga na mengine yakitoa wito wa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu.

Wahudhuriaji waliitikia wito huo kwa nguvu, wakiomba kwamba Mwenyezi Mungu (swt) awalipe kheri Mashababu wa Hizb na abariki juhudi zao.

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.