Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Upenyaji wa Mayahudi wa Jeshi la Misri

(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al-Rayah – Toleo 564 - 10/09/2025 M

Na Ustadh Saeed Fadl *

Tangu serikali ya Misri itie saini Makubaliano ya Camp David mwaka 1979, jeshi la Misri limeingia katika njia ya utegemezi na upenywaji, likijitenga na kanuni yake ya awali ya kuulinda Ummah na kulinda mipaka yake dhidi ya maadui wake wa kweli, wa kwanza miongoni mwao ni Mayahudi walioinyakua Palestina. Hatua kwa hatua, taasisi hii imebadilika na kuwa chombo kilichozuiliwa, chini ya masharti ya adui, hata kushiriki katika kuilinda na kuiwezesha kupitia mikataba ya kijeshi, usalama, kiuchumi, na ushauri ambayo iliunda utaratibu kamili wa ushawishi wa Kiyahudi, ndani ya jeshi na dola.

Hatua kuu ya mabadiliko ilikuwa Mkataba wa Camp David, ambao uliainisha kugawanya Sinai katika maeneo ya kijeshi, kubainisha idadi ya askari na aina za silaha, chini ya usimamizi wa kimataifa. Kwa hiyo, Sinai iliondolewa uwepo wowote wa kijeshi halisi wenye uwezo wa kukabiliana na adui mwenye hila mwenye kuvizia. Majeshi ya kimataifa yakawa macho wazi katika kuhudumia ya umbile la Kiyahudi linalokalia kimabavu na Amerika. Makubaliano haya yaligeuza mpaka wa mashariki wa Misri kuwa sehemu salama kwa umbile la Kiyahudi baada ya daima kuwa chanzo cha tishio kwake. Hiki ndicho kiini cha upenyaji.

Jambo hilo halikuishia kwenye mkataba huyo. Amerika, mshirika mkuu wa umbile la Kiyahudi, iliimarisha upenyaji huu kupitia usaidizi wa kimasharti wa kijeshi. Kila mwaka, jeshi la Misri hupokea vifaa vya thamani ya dolari bilioni 1.3 lakini kwa masharti kwamba kamwe lisimiliki silaha ambayo inavunja mizani ya usawa na Mayahudi, na kwamba libaki kutegemea vipuri vya Marekani, mafunzo, na msaada wa kilojistiki. Mpangilio huu ulifanya jeshi kuwa mateka kwa Amerika, na kwa hivyo kuanikwa kwa Mayahudi. Itikadi yake ya kijeshi ilibadilishwa kupitia mazoezi ya pamoja kama “Bright Star,” ambapo “ugaidi,” unaofafanuliwa kulingana na vipimo vya Magharibi, na kumaanisha Uislamu katika hali yake halisi, ukawa ndio adui, sio Mayahudi wanaoshambulia au umbilo lao vamizi. Haya ndiyo yalikuwa mabadiliko makubwa zaidi ya kimkakati katika fikra za jeshi ambalo awali liliwahi kusifiwa kama “jeshi la Ummah na ngao yake.”

Baada ya muda kupita, njia za moja kwa moja za mawasiliano zilifunguliwa kati ya ujasusi wa Misri na Mossad kwa kisingizio cha “uratibu wa usalama” huko Sinai na Gaza. Vyombo vya habari vya Magharibi, ikiwemo ni  New York Times, vilikiri kwamba ndege za umbile la Kiyahudi zilifanya mamia ya mashambulizi ndani ya Sinai, kwa idhini kamili ya Misri na uratibu kati ya 2015 na 2018. Kwa maana nyengine, jeshi la Misri halikuacha tu kulinda ardhi yake, lakini pia liliwaruhusu Mayahudi kutumia anga ya Misri dhidi ya wale wanaowaita “magaidi,” lakini ambao, kiuhalisia, ni Waislamu wanaokataa udhibiti wa Magharibi, na uwepo wa umbile vamizi.

Jeshi la Misri pia liliingia katika nyanja ya kiuchumi kupitia ushirikiano wa wazi au usio wa moja kwa moja na makampuni yenye mafungamano na umbile la Kiyahudi, hasa katika sekta ya nishati na gesi. Mnamo mwaka wa 2018, Misri ilitia saini makubaliano na makampuni ya Kiyahudi kusambaza gesi kwa viwanda vya kuzalisha gesi vya Misri kwa ajili ya kuuza tena nje ya nchi, mkataba ambao vyombo vya habari vya Kiebrania uliuita “mkataba wa karne,” ukiipa umbile hilo njia ya kimkakati ya gesi yake. Jeshi halikuwa mbali na hili, kwani makampuni yake yalijihusisha na shughuli za uzalishaji gesi na usafirishaji. Hii ina maana kwamba taasisi ya kijeshi inayodaiwa kulinda rasilimali za Ummah ikawa mshirika katika kuwawezesha Mayahudi wanaoikalia kwa mabavu kuzinyonya.

Hatari zaidi leo ni kufunguliwa kwa faili la kubinafsisha makampuni yanayomilikiwa na jeshi kama vile Wataniya Petroleum, Safi, Silo Foods, na Chill Out. Misri ilisajili makampuni ya ushauri ya kimataifa kusimamia urekebishaji na utoaji, kama vile PricewaterhouseCoopers (PwC), miongoni mwa zengine. Makampuni haya yanafanya kazi kwa uchangamfu ndani ya umbile la Kiyahudi, yakitoa huduma za kifedha na ushauri, baadhi yao moja kwa moja kwa serikali yake. Kwa hivyo, adui alipata njia ya kufikia wa maelezo ya kifedha na kimuundo ya makampuni ya jeshi, kwa njia ambayo haijawahi kuonekana hata kwenye kilele cha uvamizi halisi. Kwa hivyo, upenyaji haufungiki tena kwenye itikadi ya kijeshi na silaha, lakini umefikia muundo wa kiuchumi wa ndani wa jeshi.

Kuanzia enzi ya Sadat hadi ya Sisi, simulizi ya jeshi na vyombo vya habari rasmi iliundwa upya ili serikali ya Kiyahudi isiwe adui tena bali mshirika katika kudumisha usalama. Mnamo 2016, Sisi mwenyewe alitangaza. “Amani na ‘Israel’ ni thabiti na endelevu, na kila mtu lazima aimarishe uaminifu nayo.” Kwa hiyo, mpaka wa Misri na Mayahudi ukawa sehemu yake salama zaidi, huku jeshi likielekezwa kupigana na wana wa Ummah huko Sinai, Libya, na Sudan, chini ya bendera ya kupambana na ugaidi. Ugeuzaji huu wa itikadi unaweza tu kuelezewa kwa upenywaji kamilifu wa akili ya kijeshi ya Misri.

Upenywaji wa jeshi la Misri na Mayahudi haikuwa bahati mbaya, wala mahusiano ya kupita tu. Ni matokeo ya sera iliyopigiwa hesabu ambayo ilianza na mikataba ya kujisalimisha, ikaendelea na utegemezi wa kijeshi kwa Amerika, kupanuka hadi uratibu wa kiusalama na kijasusi, na kuzama ndani ya mtego wa kiuchumi, na kukamilika kwa ubinafsishaji wa makampuni ya kijeshi, chini ya washauri waliokita mizizi ndani ya umbile la Kiyahudi. Hii haibadilishi tu umbile la jeshi, bali pia inabadilisha nafasi ya Misri katika mlingano wa Ummah.

Enyi watu wa Misri: yaliyotokea na yanayoendelea kutokea kuanzia kusalimisha ardhi kwa adui kupitia mikataba, hadi kuitiisha maamuzi ya kijeshi na kiuchumi kwa Amerika, hadi kufungua milango ya uratibu wa usalama na Mayahudi, kuwawezesha kupata utajiri wa Waislamu na siri za taasisi kupitia mashirika yao ya ushauri ni vitendo vilivyoharamishwa na Sharia. Kwa hakika hayo ni matendo ya khiyana dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na Waumini. Mwenyezi Mungu (swt) ametuamrisha kutayarisha nguvu dhidi ya maadui zetu, na kamwe tusiwachukue kama washirika au washauri, na kulinda rasilimali na amana za Ummah, kamwe tusizikabidhi kwa adui anayekalia kimabavu au kumwezesha kuwatawala Waislamu. Kinachotokea leo ni kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) aliharamisha na kuonya dhidi yake. Sera hizi ni miongoni mwa aina hatari zaidi za uzembe na khiyana, kwani zinajumuisha kuachana na faradhi ya Shariah ya Jihad, kumtia nguvu adui, na kumsaidia kubakia katika ardhi za Waislamu, ambapo faradhi ya asili ya Shariah ni kupigana naye mpaka ardhi isafishwe kutokana na uchafu wake.

Kwa hiyo, ni wajibu kwenu, enyi watu wa Misri, watu pamoja na jeshi, kutambua uzito wa yale yanayofanywa kwa jeshi lenu na nchi yenu, na kusimama kama kitu kimoja dhidi ya upenyaji huu. Kinachotakiwa kwenu sio kunyamaza au kusalimu amri, bali ni kupaza sauti zenu na kufanya kazi ya kufuta mikataba hii batili iliyo muweka salama adui na kukufungeni pingu, na kulirudisha jeshi kwenye Aqidah yake sahihi ya Kiislamu, kwamba kupigana na Mayahudi ni faradhi ya Shariah, si khiyari. Hii lazima iwe hivyo hadi pale Palestina yote itakapokombolewa, na maamuzi ya kisiasa, kijeshi, na kiuchumi ya Misri yaachiliwe huru kutokana na utegemezi wa Amerika na Magharibi, ushawishi wote wa kigeni na makampuni yanayohusishwa na adui yafungwe, na rasilimali za Umma zirudishwe kwenye mamlaka yao halali.

Enyi Watu wa Misri: Uislamu unakufaradhishieni kusimama mbele ya jeshi lenu na kuliregesha kwenye nafasi yake halisi, jeshi la Ummah linalopigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt), sio jeshi linalosimamiwa na maamuzi au maslahi ya adui. Jueni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikupeni bishara njema kuhusiana na matokeo ya mapambano na Mayahudi aliposema: «تُقَاتِلُونَ الْيَهُودَ فَتَقْتُلُونَهُمْ، حَتَّى يَقُولَ الْحَجَرُ: يَا مُسْلِمُ، هَذَا يَهُودِيٌّ وَرَائِي فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ» “Mtapigana na Mayahudi, na mtawauwa, mpaka jiwe litasema: ‘Ewe Muislamu, huyu hapa Myahudi yuko nyuma yangu, njoo umuue.’” (Imepokewa na Muslim).

Hizi ni bishara njema yenu, hii ndiyo njia yenu, na hii ndiyo faradhi yenu ya Shariah. Msidanganywe na meza za udhalilifu au ahadi za makafiri. Njia ya heshima ni moja, kusimama juu ya msingi wa Uislamu, kuasisi mamlaka yenu huru, na kuregesha jeshi lenu kuwa upanga dhidi ya adui, sio ukuta unaomlinda.

* Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.