- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Kuinusuru Gaza, ni Wito wa Umoja kwa Watawala: “Miaka miwili imepita! Hatungojei Maneno, bali Vitendo!”
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miaka miwili kamili, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo hadi sasa yamesababisha kuuwawa shahidi, kujeruhiwa, na kupoteza zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu 240,000, Hizb utTahrir/Wilayah Uturuki, iliandaa matembezi makubwa ya halaiki katika mji mkuu wa Ankara na katika mji wa Istanbul na mji wa Şanlıurfa, yenye kichwa:
Wito wa Umoja kutoka Viwanjani kwa ajili ya Gaza katika Mwaka Wake wa Pili:
“Wito wa Umoja kwa Watawala: Miaka Miwili Imepita! Hatungojei Maneno, Bali Vitendo!”
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa pili wa “Kimbunga cha Al-Aqsa,” kilichozinduliwa na Mujahidina katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) ili kukabiliana na uvamizi na mauaji yanayoendelea kwa karne moja, Hizb ut Tahrir nchini Uturuki iliandaa visimamno na taarifa kwa vyombo vya habari jijini Istanbul, Ankara, na Şanlıurfa, chini ya kichwa “Wito wa Umoja kwa Watawala.”
Katika maandamano hayo, yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Uturuki, na kuunganishwa chini ya bendera yake na asasi nyingi za kiraia za Kiislamu kwa ushirikiano na “Baraza la Mabadiliko Msingi”, chini ya kauli mbiu “Tuungane kwa ajili ya Gaza,” katika kutetea Waislamu wasio na ulinzi walioachwa peke yao chini ya nira ya mauaji ya halaiki, kuzingirwa, na uvamizi ambao umeendelea kwa miezi 24, waandamanaji walielekeza wito wao kwa serikali ya Uturuki chini ya kauli mbiu “Miaka Miwili imepita Hatungojei Maneno, bali Vitendo!”
Maelfu ya Waislamu, wakiwemo wanaume, wanawake, na watoto, pamoja na wasomi, wahubiri, waandishi wa habari, wanaharakati, na wataalamu wa vyombo vya habari, na wanahabari walishiriki katika matembezi hayo.
Baada ya swala ya adhuhuri, matembezi yalianza kutoka Msikiti wa Muhammad Al-Fatih hadi Uwanja wa Bayezid jijini Istanbul; kutoka Msikiti wa Kocatepe hadi Uwanja wa Sehitli jijini Ankara; na kutoka Hifadhi ya Ali Çeli hadi Uwanja wa Rabaa jijini Şanlıurfa. Waislamu walitengeneza mandhari ya kihistoria huku wakiadhimisha “Kimbunga cha Al-Aqsa” na watu wa Gaza, wakiwa wamebeba bendera za tawhid, wakipiga takbira na kuimba kauli mbiu za Kiislamu.
Kila kundi katika matembezi hayo lilibeba mabango yenye ujumbe kuhusiana na Gaza. Miongoni mwa kauli mbiu zilibebwa njia nzima ni: “Amani kwa Gaza, upinzani unaendelea,” “Kimbunga cha Al-Aqsa ni kaburi la Mayahudi,” “Majeshi yaelekee Al-Aqsa,” “Sumood Flotilla iko njiani, basi meli ziko wapi?”, “Ima muiokoe Gaza au toeni njia kwa Ummah”, “Hakuna kulaani! Hakuna mazungumzo! Bali ni vitengo!”, “Hakuna kukaa! Hakuna kulala! Ni kusonga!”, “Sitakuwa mshirika wa Marekani, mimi ni Muislamu, mimi ni Muislamu”, “Anusha tawala vibaraka za khiyana”, “Majeshi na yaungane, Israel iangamizwe”, “Waumini wataunga, na Israel itashindwa”, “Alfajiri ya kweli itachomoza, na Israel itashindwa”, “Dhamiri ya kibinadamu itaushinda Uzayuni”, “Nakuitikia, nakuitikia, nakuitikia ewe Aqsa”, “Umma mmoja, dola moja, suluhisho moja: Khilafah.”
Baada ya matembezi kukamilika, hotuba na programu zilianza viwanjani. Taarifa kwa vyombo vya habari jijini Istanbul iliwasilishwa na mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Uturuki, Mahmoud Kar; jijini Ankara, iliwasilishwa na İslam Boztepe kwa niaba ya Baraza la Mabadiliko Msingi; jijini Şanlıurfa, iliwasilishwa na Sait Doğan kwa niaba ya Baraza la Mabadiliko Msingi.
Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliwahutubia watawala wa Uturuki na nchi nyengine za Kiislamu ambao wameitelekeza Gaza, ikisema: “Huku mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia wanachinjwa, munalaani na kufanya mazungumzo ya kidiplomasia yasiyo na maana. Mumetuma jumbe kwenye Twitter na kuandaa matembezi. Baadhi yenu mumechagua kuwa kimya, huku wengine wakichagua mazungumzo ya mara kwa mara. Mnajua vizuri kwamba hakuna hata moja ya hatua hizi ambazo zilichukua na kushikika na madhubuti kwa suluhisho. Kwa sasababu mazayuni wanyakuzi hwakomeshwi kwa maneno. Na mauaji ya halaiki, ambayo yataingia katika mwaka wake wa tatu, hayamaliziki kwa maneno ya hamasa. Wanaodhulumiwa Gaza haimkiniki kuwaokoa kwa maneno pekee. Kwa hivyo, umefika wakati wa vitendo sio maneno. Kinachotakiwa ni hatua madhubuti za kivitendo. Sisi hatungojei kutoka kwenu maneno bali vitendo! Hatungojei hamasa bali harakati! Hatungojei kushutumu bali adhabu!”
Taarifa hiyo pia iliorodhesha mambo tisa, ikiwa ni pamoja na hatua madhubuti na hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa Gaza. Sehemu ya mwisho, iliyopewa anuani “Enyi umbile vamizi la Kiyahudi, enyi waoga na wapotovu zaidi katika uso wa ardhi”, iliwahutubia wahusika wa mauaji ya halaiki: “Kina mama wote wa Kiislamu sasa wananyonyesha watoto wao uadui wenu. Kina baba wanawashauri watoto wao wa kiume kukung’oeni kutoka katika ardhi hiyo. Vijana wanahesabu siku za kujiunga na jeshi la Waislamu ambalo litapigana na nyinyi. Waislamu wadogo kwa wakubwa wanafanya kazi usiku na mchana kusimamisha Khilafah Rashida, ambayo itakung’oeni kutoka katika ardhi hii, itang’oa tawala zenu za kidhalimu na za mauaji, na kuwang’oa makafiri wakoloni wa Kimagharibi ambao watasimama nyuma yenu hivi karibuni, na pindi hili likiwa hivi karubuni, nyoyo za Waumini zitashangilia kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu; na nyuso za madhalimu zitakuwa nyeusi na nyoyo zao zitajaa hofu”
Baada ya kumalizika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, mwanahabari na mwandishi Ahmet Varol, Enes Yilgun wa Jarida la “Tawhid”, Ahmet Turgut Ulucak wa “Dawah ya Mtume kwa Qur'an”, Shukru Hüseyinoğlu wa Jumuiya ya “Kizazi cha Quran”, na mwandishi Dkt. Abdurrahim Şen walitoa hotuba zao jijini Istanbul. Na jijini Ankara, Abdullah İmamoğlu alitoa hotuba kwa niaba ya Baraza la Mabadiliko Msingi na Emin Agun wa Jarida la “Tawhid”. Jijini Şanlıurfa, mkuu wa Shule ya Imam Bukhari, Mullah Ibrahim Halil Kaplan, na Bw Mullah Ahmed Tokhobi, na Selim Kandemir, kwa niaba ya Jarida la “Tawhid”, msemaji wa jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali la Şanlıurfa, Ibrahim Coşkun, mkuu wa jumuiya ya “Tone la Rehema”, Imam na khatibu Muhammad Amin Kutluway, na Mkuu wa Jumuiya ya Sayansi na Misaada ya Shirazi, Seda Benyamin Kılıç, alitoa hotuba kwenye hafla hiyo.
Amali hiyo ilihitimishwa kwa dua kwa ajili ya nusra kwa Waislamu wa Gaza na ardhi zote za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
Jumapili, 6 Rabi' al-Akhir 1447 H sawia na 28 Septemba 2025 M
- Sehemu ya Matembezi hayo ya Halaiki katika Mji Mkuu Ankara -
- Sehemu ya Matembezi hayo ya Halaiki katika Mji wa Istanbul -
- Sehemu ya Matembezi hayo ya Halaiki katika Mji wa Şanlıurfa -
- Picha za Amali ya Matembezi Makubwa ya Halaiki ya Kuinusuru na Kuiombea Nusra Gaza na Palestina Yote inayokaliwa kwa mabavu -
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
https://www.hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/uturuki/5029.html?print=1&tmpl=component#sigProId64752977c4
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa X wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Chaneli ya Daily Motion ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki