- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Kisimamo cha Port Sudan cha Kutibua Mpango wa Kujitenga kwa Darfur!
Kujibu kwa takbira, tahlil, na uungaji mkono, pamoja na vyombo vya habari na uhamasishaji wa kisiasa, kisimamo kilifanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kutibua mpango wa kujitenga kwa Darfur kilifanyika mbele ya Msikiti Mkuu mjini Port Sudan. Waumini walikusanyika baada ya swala ya Ijumaa, 20 Rabi' al-Awwal 1447 H - 12 Septemba 2025 M, kwenye Msikiti Mkuu mjini Port Sudan kwa ajili ya kisimamo hicho ikiwa ni sehemu ya kampeni ya hizb kutibua mpango wa kujitenga kwa Darfur.
Wakati wa kisimamo hicho, bendera za Mtume (saw) zilipeperushwa angani, pamoja na mabango ya kutaka kutibuliwa kwa mpango wa Darfur, na kufanya kazi ya kuunganisha umma, kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutabikisha Shariah yake kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, Ibrahim Othman (Abu Khalil), alitoa hotuba kwa wasikilizaji, ambao walijibu kwa takbir na tahlil, wakipinga njama hii ya uhalifu. Walithibitisha uungaji mkono wao kwa ajili ya umoja wa Umma wa Kiislamu, kusimamishwa kwa Dini yake, na utekelezaji wa sheria ya Mola wake Mlezi, Mtukufu.
Alisema:
“Enyi watu wa Sudan: Simameni kutibua njama, kuondosha athari za vibaraka na wanafiki, na kusahihisha njia ya maisha yenu. Muumini hang’atwi mara mbili kwenye shimo moja. Tuling’atwa na shimo la Amerika kwa kuitenga kwake Sudan Kusini. Je, tuiruhusu itenganishe Darfur? Al-Bukhari na Muslim wamesimulia kutoka kwa Abu Hurayrah (ra) kwamba Mtume (saw) amesema: لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ "Muumini hang’atwi mara mbili kwenye tundu moja.”
Tovuti kadhaa za habari ziliripoti juu ya kisimamo hicho pamoja na picha kamili. Pia kilizalisha ushiriki mkubwa wa kisiasa na vyombo vya habari miongoni mwa makundi ya kisiasa na vyombo vya habari, na kuzalisha shughuli za kisiasa na vyombo vya habari ambazo zilileta suala la Darfur katika mstari wa mbele katika tahadhari ya taifa. Pengine hii itawapa motisha watiifu wa umma, wakiwemo wasomi, wanasiasa, wanahabari, na maafisa wa jeshi, kutibua njama hii ya uhalifu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu auunganishe Umma wa Kiislamu na kuunganisha neno lake ili kusimamisha dini yake katika Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hii pekee ndio inaweza kukwamisha njama za wakoloni makafiri.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Jumamosi, 20 Rabi' al Awwal 1447 H sawia na 12 Septemba 2025 M
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
https://www.hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/sudan/4975.html?print=1&tmpl=component#sigProId42da9afa7a
Kwa Maelezo Zaidi, Tafadhali Zuru Tovuti za Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Facebook: Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Youtube: Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan
Daily Motion: Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan