Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Kisimamo cha Port Sudan kwa ajili ya Kufelisha Mpango wa Kuitenganisha Darfur

Kisimamo kilichofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan ili kufelisha mpango wa kuitenganisha Darfur kilipokelewa kwa maingiliano makubwa, ikiwemo takbir, tahlil, na kuungwa mkono, pamoja na uhamasishaji wa vyombo vya habari na wa kisiasa mbele ya msikiti mkuu katika mji wa Port Sudan. Waumini walikusanyika baada ya swala ya Ijumaa mnamo 20 Rabi' al-Awwal 1447 H 12 Septemba 2025 M kwenye Msikiti Mkuu wa Port Sudan katika kisimamo kilichofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan mbele ya Msikiti huo Mkuu kama sehemu ya kampeni ya Hizb kukwamisha mpango wa kuitenganisha Darfur.

Bendera za Mtume (saw) zilipeperushwa, pamoja na mabango ya kutaka kuzuiwa kwa mpango wa Darfur, na kufanya kazi kwa ajili ya kuunganisha Ummah, kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu (swt) na kutabikisha sheria yake kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), alitoa hotuba mbele ya waliohudhuria, ambao walijibu kwa takbir na tahlil, kupinga njama hii ya uhalifu. Walithibitisha kuunga mkono umoja wa Umma wa Kiislamu, kusimamisha dini yake, na utabikishaji wa sheria ya Mola wake Mtukufu.

Miongoni mwa mambo aliyoyasema katika hotuba yake ni:

Enyi watu wa Sudan, simameni kukwamisha njama hiyo, tokomezeni athari za vibaraka na wanafiki, na sahihisheni njia ya maisha yenu. Muumini hang’atwi mara mbili kweny shimo moja. Tuling’atwa kutoka shimo la Amerika kwa kujitenga kwa Sudan Kusini. Je, tuiruhusu kutenganisha Darfur?! Imepokewa kutoka kwa Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu Hurairah (ra) kwamba Mtume (saw) amesema:

“لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ”

“Muumini hang’atwi mara mbili kwenye shimo moja.”

Tovuti kadhaa za habari ziliripoti juu ya kisimamo hicho, zilizo andamana na picha. Pia maingiliano mkubwa ya kisiasa na vyombo vya habari yalitokea miongoni mwa makundi ya kisiasa na vyombo vya habari, na kuzalisha harakati za kisiasa na vyombo vya habari ambazo zililifanya suala la Darfur kuwa mstari wa mbele katika usikivu wa nchi. Pengine hili litawapa motisha miongoni mwa wenye ikhlasi katika wana wa Umma katika wanazuoni, wanasiasa, wanahabari na maafisa wa jeshi kutibua njama hii ya kihalifu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu auunganishe Umma wa Kiislamu na kuunganisha neno lake ili kusimamisha dini yake katika dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hiyo ndio pekee inaweza kukwamisha mipango ya makafiri wakoloni.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

Jumamosi, 20 Rabi' al-Awwal 1447 H sawia na 12 Septemba 2025 M

Kwa Maelezo Zaidi, Tafadhali Zuru Tovuti za Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya Daily Motion ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.