- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Indonesia:
Matembezi Makubwa ya Kukumbusha Ulimwengu “Palestina ingali chini ya Uvamizi”
Maelfu ya Waislamu katika miji mbalimbali ya Indonesia walifanya matembezi yanayounga mkono Palestina mnamo Oktoba 18 na 19, 2025, chini ya kauli mbiu “Palestinaingali chini ya Uvamizi.” Huko Bandung, zaidi ya waandamanaji 15,000 walikusanyika mbele ya jengo la Gedung Sati, wakinyanyua bendera za Rayah zenye tamko la Tawhid na mabango yenye kauli mbiu kama vile “Tumeni majeshi ya Kiislamu, yakomboe Palestina!”, na “Suluhisho la mwisho kwa Palestina ni kupitia jihad na Khilafah,” na “Palestina itakombolewa kupitia Khilafah na Jihad.”
Wazungumzaji walisisitiza kwamba usitishaji mapigano wa sasa ni dhaifu sana, kwani wavamizi wa Kizayuni wamekiuka makubaliano mara kwa mara. Waliwasihi Waislamu kujifunza kutokana na historia, wakibainisha kuwa makubaliano ya amani na Wazayuni hayaleti faida yoyote, na wakarudia kwamba njia ya kweli ya kuikomboa Palestina iko katika jihad, kama ilivyoamriwa na Quran Tukufu.
Matembezi mithili ya hayo yalifanyika Semarang na Purwokerto, huku maelfu ya watu kutoka maeneo jirani wakishiriki. Waandamanaji walibeba mabango yaliyopinga suluhisho la dola mbili, wakiliona kuwa suluhisho la uongo linaloendeleza uvamizi. Wasomi wa kidini na viongozi wa jamii walilaani kimya cha watawala wa Waislamu, wakikielezea kama usaliti wa Uislamu na mateso ya Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa (Palestina). Walisisitiza kwamba bila umoja chini ya uongozi mmoja wa Kiislamu—Khilafah Rashida kwa Njia ya Mtume—uvamizi wa ardhi iliyobarikiwa (Palestina) utaendelea.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Indonesia
Jumatatu, 5 Jumada al-Awwal 1447 H sawia na 27 Oktoba 2025 M

- Sehemu ya Matembezi Makubwa katika Miji ya Indonesia -

Picha za Matembezi Makubwa ya Kuukumbusha Ulimwengu
“Palestina ingali chini ya Uvamizi”
https://www.hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/indonesia/5101.html?print=1&tmpl=component#sigProId3532aed390

- Alama Ishara za Amali za Kuinusuru Gaza -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies

Kwa Maelezo zaidi Tafadhali Zuru:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Indonesia
