Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tanzia ya Mwanachama wa Afisi ya Amiri,

Ustadh Ahmad Bakr (Abu Osama)

(Imetafsiriwa)

[مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]

Amiri wa Hizb ut Tahrir, Wanachama wa Afisi ya Amiri, Diwani ya Al-Madhalim (Malalamiko), na Afisi Kuu ya Habari na Hizb ut Tahrir kwa jumla wanaomboleza kwa Umma wa Kiislamu Mwanachama wa Afisi ya AmIrI, Ustadh Ahmad Bakr (Abu Osama) aliyefariki dunia asubuhi ya leo, 22 Rabi’ Al-Awwal 1447 H sawia na tarehe 14 Septemba 2025 M, akiwa na umri wa miaka themanini na saba.

Abu Usama alitokana na kizazi cha kwanza cha Hizb ut Tahrir ambaye alibeba Dawah kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida. Alibaki imara juu ya haki na akaubeba ulinganizi huu hadi kifo chake. Hakutishwa na tawala na dhulma zao, wala na jela za kutisha za wakandamizaji kama vile magereza ya Hafez na Bashar al-Assad, ambako aliteseka kwa miaka mingi! Alipoachiliwa huru kutoka gerezani, hakuwa mvivu wala hakushindwa, bali aliendelea na njia yake katika kubeba ulinganizi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nguvu na uthabiti wa wanaume wa kweli, macho yake yakiwa na shauku ya pambazuko la Khilafah na utabikishaji wa Uislamu kwa itikadi na mfumo wake... Hata hivyo, Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu, amemchagulia kilicho kikubwa na bora zaidi, kwa ridhaa yake, utukufu ni wake Yeye.

 [فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِنْدَ مَلِيكٍ مُقْتَدِرٍ] “Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.” [Al-Qamar: 55].

Mwenyezi Mungu akurehemu, Abu Usama. Tumehuzunishwa na kuondoka kwako, na tunasema tu yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt).

[الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 156]. Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake Yeye tutarejea.

Ndugu Yenu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, haswa

Na Wanachama wa Hizb ut Tahrir, kwa jumla

22 Rabi’ al-Awwal 1447 H 

14 Septemba 2025 M

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.