Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 29 Dhu al-Qi'dah 1446 | Na: HTY- 1446 / 22 |
M. Jumatatu, 02 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sheria ya Kimataifa ni Sheria ya Pori - Hairuhusiwi Kuiendea
[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ]
“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Surat Al-Ma’idah: 50]
(Imetafsiriwa)
Chini ya ufadhili wa Daniel Capoli, Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu katika misheni ya Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) nchini Yemen, ICRC huko Sana'a ilipanga, mnamo Jumanne na Jumatano, 20-21/05/2025, kwa ushirikiano na Wizara ya Habari na Wizara ya Mambo ya Nje, kozi ya mafunzo katika Wizara ya Mambo ya Nje kwa wafanyikazi wa vyombo vya habari na taasisi ya waandishi wa habari. Kozi hiyo ilishughulikia sheria za kimataifa, misingi na malengo yake, na istilahi zinazohusiana na sheria za kimataifa za kibinadamu, haswa katika suala la haki za binadamu katika ulinzi na maisha yenye staha, kuzuia ghasia, na kukidhi mahitaji ya vikundi vilivyo hatarini zaidi vinavyofinikwa na ulinzi wake, na vile vile kulinda raia dhidi ya athari za uhasama na kuharamisha mateso yasiyo na haja au madhara kupita kiasi.
Kilichojitokeza katika kozi ya mafunzo ya sheria za kimataifa ni ushiriki wa Naibu Waziri wa Habari, Dkt Omar Al-Bukhaiti, ambaye alitoa wito wa kuanzishwa kanuni na misingi yake kati ya wanataaluma wa vyombo vya habari wa Yemen. Alisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kuangazia kanuni msingi za sheria ya kimataifa ya kibinadamu, na kusifu usaidizi wa kuendelea wa ICRC nchini Yemen katika kuandaa programu kama hizo za uhamasishaji zinazohusiana na kanuni, misingi, na malengo ya sheria hii ya kibinadamu na katika kuanzisha sheria zake. Aliisihi kamati hiyo kuzidisha kozi hizo kwa wanahabari nchini Yemen. Pia walioshiriki ni Mkuu wa Taasisi ya Diplomasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Dkt Ahmed Al-Imad, Mshauri wa Kisheria wa ujumbe wa ICRC nchini Yemen, Mohammed Al-Nazili, na msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Waheed Al-Shami. Wote walizungumza katika semina hiyo kuhusu kufafanua sheria za kimataifa, kanuni na fahamu zake, kueneza ufahamu, na kuimarisha kanuni zake.
Haya yote yalifanyika katika ardhi ya imani na hekima Yemen, kwa baraka za wale walio mamlakani jijini Sana'a wanaojiita Ansar Allah! Hivyo basi, mapinduzi yalikuwa kwa ajili ya nini? Vipi kuhusu madai ya mabadiliko na ujenzi? Vipi kuhusu kauli mbiu tupu, za uwongo?!
Sheria ya kimataifa ilianzishwa kwa uadui kwa Uislamu na Waislamu katika awamu zake zote: 1648, 1919, na 1945. Kwa hiyo, mawazo yake yoyote hayapaswi kutekelezwa katika ardhi za Kiislamu, wala kukuzwa au kulinganiwa. Inapingana na itikadi ya Kiislamu na masuluhisho yote yanayotokana nayo kushughulikia matatizo ya maisha ya mwanadamu. Je, Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia havikufanywa chini ya sheria hii ya kimataifa?
Je, vita kati ya Waislamu kwa Waislamu nchini Yemen havijadumu kwa miaka 11 chini ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa, chini ya Sura ya VII, chini ya pazia la kudumisha amani ya kimataifa? Na je, mauaji ya halaiki mjini Gaza yanayokaribia miaka miwili pia hayafanyiki chini ya uangalizi wa sheria hii hii ya kimataifa?
Katika Uislamu, mahusiano kati ya nchi yanatokana na mgawanyiko wa dunia kuwa Dar al-Islam (Ardhi ya Uislamu) na Dar al-Harb (Ardhi ya Vita), sio kwa msingi wa sheria za kimataifa. Mahusiano baina ya dola yanatokana na usawa na ubadilishanaji wa usawa, si mfumo ambapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina matabaka mawili ya wanachama: wale wa kudumu wenye kura ya turufu, na wale wasio wa kudumu wasio nayo!
Hizb ut Tahrir ina ruwaza ya wazi iliyojengwa juu ya msingi wa Sharia ya sera ya kigeni na mahusiano ya kimataifa, kama ilivyo kwa mifumo ya utawala, uchumi, jamii, na mengineyo, kupanga mambo ya maisha chini ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Ama kuwaridhisha makafiri, kufuata nyayo zao, na kuchukua msaada kutoka kwao, huko ni kujiua kisiasa, khiyana ya wazi, na uhaini dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Sisi katika Hizb ut Tahrir tutaendelea kuwafichua vibaraka wahalifu, kuongeza ufahamu miongoni mwa wana wa Ummah, kukabiliana na kafiri Magharibi na vibaraka wake, kusimama nao, na kuuongoza Ummah kuelekea lengo lake kuu: kuregesha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida.
[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ] “Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Surat Yusuf:21]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.hizb-ut-tahrir.info |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |