Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  2 Jumada I 1447 Na: 04 / 1447
M.  Ijumaa, 24 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tafakari Muhimu Kuhusu Taarifa ya Chama cha Maimamu nchini Uholanzi

(Imetafsiriwa)

Taarifa ya Chama cha Maimamu nchini Uholanzi (VIN) inadai kwamba ushiriki wa kisiasa ndani ya jamii za Ulaya ni “njia inayoruhusiwa na halali,” na kwamba ushiriki unaweza hata wa kupendekezwa au wa lazima kulingana na hali. Msimamo huu unahitaji kuzingatiwa kwa makini, kwani unaegemezwa juu makisio ambayo hayaakisi vya kutosha uhalisia wa mfumo wa kisekula.

Usekula sio tu utenganishaji dini na siasa, lakini pia unaamuru ni dori gani dini inaruhusiwa kucheza katika jamii. Kwa hivyo sio muundo usioegemea upande wowote ambapo Waislamu wanaweza kulinda haki zao tu, bali ni utaratibu wa kifikra wenye sheria zake. Katika utaratibu huu, sheria haikujengwa juu ya wahyi bali yote inaachwa kwa maamuzi ya mwanadamu, kulingana na wengi wanaobadilika.

Kwa kweli, usekula ni kama dini mpya: dini ambayo chanzo cha sheria sio wahyi tena, bali mwanadamu mwenyewe ameinuliwa hadi chanzo kamili. “Dini” hii sasa inatawala duniani kote, ikiwemo katika nchi za Kiislamu, ambapo imebadilisha sheria za Kiislamu. Hii imesababisha kung'oa, mgawanyiko, na kudhoofika kwa kitambulisho cha Kiislamu. Kwa wengi, Uislamu umedogoshwa hadi kuwa jambo la kibinafsi au la kiroho, huku ruwaza yake pana kama mfumo kamili wa maisha ikififia.

Inawezekanaje basi kwamba maimamu, wanaofahamu uhalisia huu, bado wawaite Waislamu kushiriki katika mfumo huu? Wanawezaje, wakiwa na ufahamu kamili wa matokeo mabaya ambayo usekula umeleta katika ulimwengu wa Kiislamu—ukoloni, mgawanyiko, ukandamizaji, na usaliti—kutumia minbar ya msikiti kuelekeza Ummah kwenye njia hiyo hiyo?

Wanatumaini kuepuka madhara gani, na wanafikiria kupata manufaa gani, kwa kuwaongoza Waislamu katika mfumo ambao lengo lake kuu ni kutengwa na kupambana na Uislamu? Mtu anawezaje kutafuta wokovu katika utaratibu ambao wenyewe unahusika kwa udhalilishaji, mgawanyiko, na ukandamizaji wa Waislamu duniani kote? Je, hawaoni kwamba ni usekula hasa ndio umesababisha udhalilishaji wa Ummah?

Hasa katika enzi hii ya ung'oaji, maimamu wana wajibu wa kuwakumbusha Waislamu kuhusu matarajio yao ya kweli: kurudi kwa Uislamu kwa ukamilifu, mfumo badali wa usekula unaofeli. Uislamu si imani ya kiroho tu bali ni mfumo kamili unaojumuisha siasa, uchumi, jamii, na sheria.

Ingekuwa ni heshima kwa maimamu kutoa wito kwa jamii bila kusita katika njia hii—sio kwa kuwahimiza kujiyeyusha ndani ya mfumo wa kisekula, bali kwa kuwatia moyo kubaki waaminifu kwa msingi wao na kufanya kazi kwa ajili ya kuregea kwa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha.

Huu sio wito wa kutojali, kwani Waislamu wanaweza kuzifanya sauti zao zisikike na kutoa shinikizo bila kulegeza msimamo na bila kupunguza maadili yetu kwenye muundo wa kisekula. Hatua halisi haiko katika kutoa kura yetu ndani ya mfumo unaoutenga Uislamu, bali katika kuimarisha sauti yetu ya pamoja na kushikamana kwa uthabiti na kanuni zetu wenyewe.

Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.