Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 29 Rabi' I 1447 | Na: 1447/02 |
M. Jumapili, 21 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani Yaendesha Uharibifu... Na Watawala ni Watiifu kwa Miradi Yake ya Kikoloni!
(Imetafsiriwa)
Mamlaka zilizofuatana juu ya nchi yetu hazikujiepusha na kutii mashinikizo ya Marekani, kwa kukubali kushiriki katika kuimarisha mkakati wake wa kikoloni katika kuitawala dunia nzima, ikiwemo kanda yetu ya Waarabu na eneo letu la Afrika. Hii ni kama vile kusainiwa na utawala wa Sebsi juu ya uamuzi wa Barack Obama wa kuipa Tunisia hadhi ya Mshirika Mkuu Asiyekuwa mwanachama wa NATO, au kufungua nchi yetu kwa mpango wake barani Afrika kwa kuandaa, kwa mwaka wa nane mfululizo, mazoezi ya kijeshi ya African Lion 2025, ambapo Jenerali Dagvin Anderson, kamanda wa Kamandi ya Marekani ya Umoja wa Mataifa Afrika (AFRICOM) alisema mbele ya Kamati ya Huduma za Silaha katika Bunge la Congress la Marekani kwamba Morocco na Tunisia ni miongoni mwa washirika wenye uwezo mkubwa wa kusafirisha usalama barani humo. Na kama upanuzi wa kupenya huku kwa Marekani, ilikuja katika tovuti ya TUNISIE TELEGRAPH kwamba wiki ijayo nchini Tunisia itazinduliwa mafunzo ya hali ya juu yaliyobobea katika kukabiliana na hatari za kemikali, kibaolojia, radiolojia na nyuklia (CBRN), chini ya usimamizi wa timu maalumu kutoka Shirika la Kupunguza Tishio la Ulinzi la Marekani (DTRA), ambapo Kikosi cha 61 cha Uhandisi cha Jeshi la Tunisia kitashiriki ndani ya mipaka ya ushirikiano wa pande mbili.
Na katika kile kilicho katika habari zilizotangazwa na kamandi ya jeshi la majini la NATO, juu ya kuwasili kwa meli za operesheni ya baharini “Mlinzi wa Bahari” kwenda Tunisia na ushiriki wa Jeshi la Wanamaji la Tunisia katika kozi maalum ya mafunzo iliyoandaliwa na Kituo cha Mafunzo ya Operesheni ya Uzuiaji wa Bahari ya NATO nchini Ugiriki, katika kipindi cha 02 hadi 12 Septemba, sio chochote ila ni thibitisho dhahiri la kiwango cha hatari kubwa ambayo wanasiasa mtawalia juu ya utawala wetu waliburuza juu yetu na juu ya nchi, na utegemezi ambao walitufunga nao, huku wakijigamba juu ya ubwana na kuuhifadhi!
Na mbele ya operesheni hii ya upotoshaji, ambapo shughuli hii iliwekwa chini ya jina la “ushirikiano wa kijeshi na kiusalama” kati ya Tunisia na Amerika, na mbele ya habari hii, basi sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia tunawakumbusha watu wetu katika ardhi ya mzeituni kwa ukweli ufuatao:
Marekani, ambayo inadai kwamba inafanya kazi katika kujenga imani na sisi na kuongeza utayari wetu wa utendaji kazi, ndiyo iliyoisaliti Qatar kwa kuruhusu umbile la Kiyahudi kuishambulia Doha, na usaliti wa ujumbe wa mazungumzo wa Hamas. Na kura ya turufu ya Marekani ndiyo iliyosimama mnamo Alhamisi tarehe 18 Septemba 2025, na kwa mara ya sita, uamuzi wa Baraza la Usalama la kutaka kusitishwa mara moja, na kwa kudumu na bila masharti vita vya Gaza, pamoja na kuondoa vikwazo vya kuwasili kwa misaada ya kibinadamu kwa watu wetu wanaoteseka huko Gaza kwa mashini ya mauaji Waislamu ya Wazayuni na misimamo ya kufedhehesha ya watawala wa Waislamu.
Marekani hasa baada ya tarehe saba Oktoba 2023, ilifichua uadui wake na udunishaji wake wa damu ya Waislamu mjini Gaza na Ukingo wa Magharibi na nchini Lebanon na Iran na Yemen na Syria na hivi karibuni “mshirika” wake Qatar, na kutangaza wazi uungaji mkono wake kwa umbile la Kiyahudi katika kila sehemu ya ardhi ya Waislamu ambayo mkono wake wa khiyana unafika.
Na pia ilisaidia umbile hili la uhalifu kwa fedha na silaha na zana, na kuunga mkono uhalifu wake kwa mazungumzo rasmi ya kisiasa na kifuniko cha sheria, na kuzuia maamuzi yote ya kulaani dhidi yake. Bali ilitekeleza mashinikizo kwa washirika wake wa Ulaya na wafuasi wake Waarabu dhidi ya kila jaribio la kuvunja kutengwa kwa watu wetu huko Gaza au kuchukua misimamo huru dhidi ya umbile la Kiyahudi au wahalifu wa kivita kutoka kwa viongozi wake. Haikuacha fursa isipokuwa kwamba iliunga mkono ndani yake jinai zake na kuthibitisha ushirikiano wake kamili nalo katika vita vya maangamizi ambavyo vinawafanyia watu wetu nchini Palestina.
Wiki mbili zilizopita, sio mbali na sisi katika nchi jirani ya Libya, Marekani ilifichua katika mkutano wa siri wa Roma udhibiti wake kamili katika eneo la Libya kwa kuimarisha mgawanyiko na kugawanya dori na ngawira kwa washirika wa nje ya nchi na uongozi mpya ndani, kwa kukosekana kabisa majirani wa Tunisia, Algeria na Misri katika mchakato wa kisiasa na usalama kwamba wao ndio wa kwanza kuhusika ndani yake.
Tunisia haikutengwa na tishio na kutikiswa na vikwazo vya kiuchumi na kisiasa, huku viongozi wake wa kisiasa bado wanajishughulisha na kushiriki katika ujanja na mafunzo mengi ambayo Amerika inaendesha katika eneo hilo, ambayo malengo yake ya kikoloni yalifichuliwa, ambayo ni udhibiti wa mwambao wa kusini wa Bahari ya Mediterania na ulinzi wa Ukingo wa Magharibi wa Palestina ili kuendeleza mradi wa makaazi ya Mayahudi na kuzuia uwezekano wowote wa vikosi vya Umma kuungana pamoja kunusuru watu wetu huko Gaza na kukomesha mashini ya mauaji ambayo Mayahudi wanatekeleza kwa idhini ya Amerika.
Enyi watu wa Tunisia, enyi kizazi cha mujahidina:
Sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia tunathibitisha katika kila tukio ambalo vikosi vya majeshi yetu vinashiriki pamoja na majeshi ya Marekani, kwamba ushirikiano na adui huyu, ambaye anatangaza wazi uadui wake dhidi yetu na kuwavizia watu wetu na kutamani ardhi yetu, hautarajiwi kutoka humo kheri yoyote. Na kwamba ushiriki wake katika wakati wa vita ni uhalifu ambao kwa miaka na vikaka hautafutika. Na kwamba kuyatumia majeshi yetu kwa ajili ya kutumikia ajenda yake ni fedheha kwa maafisa wetu na askari wetu ambao wanatamani kama vile Waislamu wengine kuinusuru Dini yao na kuulinda Ummah wao na ardhi yao na matukufu yao.
Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَلاَ تَرْكَنُواْ إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللّهِ مِنْ أَوْلِيَاء ثُمَّ لاَ تُنصَرُونَ]
“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud: 113].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |