Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  24 Dhu al-Hijjah 1446 Na: 1446/15
M.  Ijumaa, 20 Juni 2025

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Ustadh Hassan Nouair

[مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia inaomboleza kifo cha mmoja wa watu wake miongoni mwa Wabebaji Da’wah, Ustadh Hassan Nouair, aliyefariki dunia leo, Ijumaa, tarehe 24 Dhu al-Hijjah 1446 H, sawia na 20/06/2025 M, baada ya mapambano na maradhi ambayo yalidhoofisha mwili wake lakini hayakuzima moto wa ujumbe wake wala azma yake ya kufanya kazi katika safu za wale wanaojitahidi kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilfah Rashida kwa njia ya Utume.

Ami Hassan Nouair, Mwenyezi Mungu amrehemu, alichukua uhariri wa Gazeti la At-Tahrir, na hakulegeza msimamo juu ya neno la haki, na wala hakuogopa lawama za wenye kulaumu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa makala yake, aliandika misimamo ya heshima adimu, na kwa ukweli, alikabiliana na udhalimu wa batili. Katika ugonjwa wake wa mwisho, alibaki mwaminifu kwa agano la neno la haki ambalo halibembelezi wala kukaa kimya wakati wa ukimya.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amkubalie miongoni mwa watu wema, aipandishe daraja yake katika daraja za juu zaidi, na awajaalie familia yake, jamaa zake, wapenzi wake na maswahaba zake wote katika njia, subira, uthabiti, na malipo.

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara 2:156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.