Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  5 Rabi' I 1447 Na: 1447/14
M.  Alhamisi, 28 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wilaya ya Al-Arish Mina, Warraq Mpya
Kuwahamisha Wakaazi wake: Uwekezaji wa Lazima au Uhalifu wa Uhamishaji?

(Imetafsiriwa)

Siku hizi, mji wa Al-Arish unashuhudia sura mpya ya mateso wanayopata wananchi wa Misri mikononi mwa utawala unaowaona watu kuwa kikwazo tu kwa mipango yake ya uwekezaji na miradi yenye faida. Baada ya kimya cha miaka mingi na ahadi za uwongo kwamba wakaazi wa wilaya ya Mina kwamba hawatadhurika, watu walishangazwa kukuta matingatinga ya serikali yakiregea kubomoa nyumba na kung’oa wakao yao, bila kujali utakatifu wa nyumba, utu, au haki za watu, ambazo Mwenyezi Mungu (swt) amewapa katika ardhi na mali zao.

Tangu Julai 2025, serikali hiyo imekuwa ikitekeleza awamu ya nne na ya tano ya mpango wa upanuzi wa Bandari ya El Arish. Imelenga takriban nyumba 180, kati ya zaidi ya nyumba 1,000 za makaazi na biashara ambazo ziko ndani ya wigo wa “manufaa ya umma” yaliyotangazwa na serikali. Ubomoaji huo ulifuatiwa na maandamano makubwa kutoka kwa wakaazi, ambao waliimba dhidi ya uhamishwaji kwa nguvu. Vikosi vya polisi vilijibu kwa ukamataji na shinikizo la kisaikolojia, mandhari ambayo imekuwa ya kawaida kila wakati serikali inapoamua kuhamisha eneo kwa ajili ya wawekezaji au miradi isiyowanufaisha wakaazi.

Ingawa serikali ilitangaza njia badali na fidia, kama vile viwanja vidogo vya ardhi au vyumba katika maeneo mengine, wakaazi waliona ofa hizi kuwa zisizo za haki na zisizo na usawa kwa thamani ya ardhi, ambayo iko eneo la kimkakati. Hii inafungua mlango mpana kwa uwekezaji mkubwa wa siku zijazo katika bandari na maeneo yanayozunguka, huku faida ikimiminika kwenye mifuko ya wachache wanaonasibishwa na serikali, huku wakaazi wa kiasili wakiachwa solemba kwa mambo hayo.

Inajulikana vyema kuwa bandari ya Arish imekuwa kivutio cha serikali tangu ilipounganishwa na Eneo la Kiuchumi la Mkondo wa Suez. Mazungumzo yameanza ya mabilioni ya pauni za uwekezaji ili kuipanua na kuibadilisha kuwa lango la kusafirisha malighafi ya madini na bidhaa zengine. Mradi huu hautofautiani kimaumbile na kuhamishwa kwa wakaazi wa Pembetatu ya Maspero katikati mwa Cairo, ambapo eneo hilo liligeuzwa kuwa eneo la uwekezaji lenye matarajio kwa kampuni kuu za mali isiyohamishika baada ya kufurushwa kwa wakaazi wake masikini. Pia haina tofauti na mkasa wa Kisiwa cha Warraq, ambapo wakaazi wamekuwa wakiishi kwa miaka mingi huku kukiwa na vitisho vya mara kwa mara na majaribio ya kufurushwa kwa nguvu yenye lengo la kukikabidhi kisiwa hicho kwa Imarati na wawekezaji na makampuni ya kigeni kwa kisingizio cha “maendeleo”.

Kile ambacho kesi hizi zote zinafanana ni kwamba kila eneo ambapo serikali inaona fursa ya uwekezaji inageuka kuwa ardhi inayotishiwa, wakaazi wake wanakuwa wahasiriwa wa kufukuzwa kwa nguvu. Serikali haijioni tena kuwa mlinzi wa mambo ya watu au mdhamini wa maslahi yao. Badala yake, imekuwa dalali, kuuza ardhi na kuwachukulia wamiliki wake kana kwamba ni wanadamu wa ziada wa kutupwa kwa ajili ya manufaa ya mipango ya masoko na matakwa ya mabepari.

Kinachofanyika ni shambulizi la waziwazi dhidi ya haki za watu na ukiukaji wa wazi wa hukmu za Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) aligawanya umiliki katika aina tatu: wa kibinafsi, wa umma, na wa dola; kila moja una sheria na mipaka yake. Ardhi zinazokaliwa na watu na kurithiwa kutoka kizazi hadi kizazi ni mali ya watu binafsi, serikali haiwezi kuwanyang'anya isipokuwa kwa sababu halali, kama vile ikiwa ardhi imeachwa bila kutunzwa au kutumika kuleta madhara ya kihakika kwa wengine. Hata hivyo, ikichukuliwa kwa nguvu kwa kisingizio cha “maendeleo” au “manufaa ya umma” na kisha kukabidhiwa kwa wawekezaji na wafanyibiashara, huku ni kula mali za watu kwa dhulma. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ]

“Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe.” [An-Nisa: 29].

Zaidi ya hayo, kuwahamisha watu kutoka katika nyumba zao na kubomoa nyumba zao kwa nguvu ni dhulma ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameiharamisha kabisa. Ni dhulma kubwa ilioje hiyo inayofanywa na mtawala anayepaswa kuwa mlinzi wa raia wake!

Zaidi ya hayo, “manufaa ya umma” ambayo serikali inataja hayana msingi katika Shariah kwa maana hii isiyo ya wazi. Bali, ni fahamu iliyoingizwa kutoka katika mifumo ya kibepari ili kuhalalisha kunyimwa haki kwa kisingizio cha maslahi ya juu zaidi yanayoamuliwa na mtawala kulingana na maslahi yake mwenyewe. Katika Uislamu, kigezo cha vitendo ni Shariah, si maslahi binafsi au uwekezaji tu. Ingawa kuanzisha bandari au kupanua mradi kunawanufaisha Waislamu, hilo kamwe halihalalishi kuwadhulumu watu au kuwanyang'anya mali zao kwa dhulma.

Katika Uislamu, ikiwa ardhi ni mali ya umma, kama vile mito, madini, na huduma vikuu vya huduma, ni milki ya raia wote, na dola ndiyo yenye jukumu la kuisimamia na kuigawanya kwa usawa. Hata hivyo, kwa serikali kuwa chombo cha kuwahamisha watu na kukabidhi ardhi zao kwa makampuni, ni kitendo kisichostahili kufanywa, kukubalika au kuvumiliwa.

Kinachotokea katika Al-Arish, Warraq, na Maspero ni kiungo kimoja tu cha silsili ndefu ya sera za serikali zinazolenga kuifunga Misri na miradi ya kimataifa ya uwekezaji na kuigeuza ardhi na watu kuwa zana katika kuhudumia njama za mabepari wa ndani na nje. Hii inaeleza kwa nini mandhari hii inarudiwa kila mahali kuna thamani ya kiuchumi inayokuja: nyumba zinabomolewa, watu wanahamishwa, dili zinafungwa, na “fidia” ndogo hutolewa kama hongo ili kuficha uhalifu huo.

Suluhu la suala hili linaweza kupatikana tu kwa kuzipinga sera hizi kutoka mizizi yake, kung’oa utawala unaozitekeleza na kuwalazimisha watu kujisalimisha kwazo, na kusimamisha Khilafah inayotawala kwa mujibu wa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, inayolinda mali za watu, kuzuia dhulma, na inasimamia vituo vya umma kwa namna ambayo inahudumia maslahi ya watu, na sio makampuni.

Kinachowatokea watu wa Al-Arish leo kinapaswa kuwa kengele ya onyo kwa watu wote wa Misri. Yeyote anayefikiri kwamba uhamishwaji utafungika kwa eneo maalum amekosea. Kila kipande cha ardhi kinachochukuliwa kuwa biashara ya pato kubwa na serikali kiko chini ya tishio, na kila familia inayoishi kwenye ufuo, kisiwa, au katikati mwa jiji lililoahidiwa kwa ajili ya “maendeleo” inatishiwa kufukuzwa. Kama vile watu wa Maspero walivyofukuzwa kutoka kwenye nyumba zao, na kama vile watu wa Warraq wamekuwa wakikandamizwa kwa miaka mingi, watu wa Al-Arish wanakabiliwa na hatima hiyo hiyo.

Enyi Watu wa Kinanah (Misri): Mkono wa serikali hii ambao haukuishia kwenye Kisiwa cha Warraq, hautatosheka na eneo la Al-Arish pekee, bali utaenea hadi kwenye kila kipande cha ardhi ambako kuna hata dalili ya tofauti na uwezekano wa uwekezaji, na utakinyakua kwa nguvu na mabavu. Kusimama kwenu dhidi ya serikali sasa na kuizuia isiwavamie na kuwashambulia watu wa Al-Arish na kunyakua ardhi yao ni wajibu wa Shariah. Mukiwatelekeza leo, serikali itakutengeni mmoja baada ya mwengine, na siku hiyo mutasema, “Nililiwa siku ile fahali mweupe alipoliwa”. Tulivamiwa siku tulipowaacha watu wa Al-Arish peke yao ili kukabiliana na serikali. Basi, tangazeni msimamo wa umoja dhidi ya utawala usioheshimu udugu wala agano nanyi, ambao unafuja haki zenu na mali zenu, unaokupigeni vita katika ardhi yenu na riziki zenu, na unaotangaza vita dhidi ya Dini yenu.

Enyi wenye ikhlasi katika jeshi la Kinanah (Misri): Ibn Taymiyyah, Mwenyezi Mungu amrehemu, alipokuwa kwenye jela yake jijini Damascus, muuwaji alimjia na kumwambia: “Nisamehe ewe sheikh wetu, kwani mimi niko chini ya amri.” Ibn Taymiyyah akamjibu, “Wallahi, lau sio wewe, wasingelidhulumu.” Wallahi, lau si nyinyi, serikali isingeitesa Misri na watu wake, wala isingeweza kuwadhulumu, wala isingeweza kuwafanya watumwa kama inavyofanya hivi sasa. Wallahi mtahesabiwa Siku ya Kiyama, siku ambayo Mwenyezi Mungu (swt) atakuiteni.

[وَقِفُوهُمْ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ * مَا لَكُمْ لا تَنَاصَرُونَ]

“Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa.” [As-Saffat: 24]

Si yenyewe, wala fedha zake, wala vyeo vyake na fadhila, ambazo kwazo inakuvutieni na ambazo kwazo inanunua Dini yenu, heshima yenu na uadilifu wenu, hazitakunufaisheni. Basi jiandaeni kwa ajili ya siku mtakapokutana na Mwenyezi Mungu (swt) huku watu wakining’ing’inia katika shingo zenu wakisema: “Ewe Mola Mlezi, wametutelekeza na wamempa nguvu adui yako na adui yetu juu yetu!” Na jueni, enyi askari wa Kinana (Misri), kwamba wajibu wenu ni kuwalinda watu dhidi ya ukatili wa serikali hii. Wajibu wenu wa kimsingi unaodhamini haki na utu wa watu ni kuung’oa utawala huu kutoka katika mizizi yake pamoja na zana zake zote, nembo na watekelezaji wake, na kuwanusuru wale wanaofanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume; jambo ambalo litawalinda watu dhidi ya ukatili wa kila dhalimu na kuwarudishia heshima na fahari yao. Hii ni dori yenu na huu ni wajibu wenu ambao kwao mtaulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Basi fanyeni hima, Mwenyezi Mungu akukubalieni na akusameheni kwa yale yaliyopita na afungue njia kupitia kwenu ili tuione kiuhalisia unaomridhisha Mwenyezi Mungu (swt) na sisi sote, na kupitia kwenu Misri itang’ara, Mwenyezi Mungu akipenda.

[وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُمْ بَيْنَكُمْ بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقاً مِّنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua.” [Al-Baqarah: 188]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.