Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  6 Rabi' II 1447 Na: 1447/15
M.  Jumapili, 28 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Wanajeshi wa Misri (Kinana): Vivuko vya Gaza havihitaji Malori, Bali vinahitaji Majeshi na Magari ya Kivita
(Imetafsiriwa)

Hali ya kibinadamu mjini Gaza imefikia viwango vya maafa ambavyo havijawahi kushuhudiwa. Idadi ya vifo vya mashahidi imezidi 65,000. Ripoti za kimataifa zinaweka idadi hiyo kuwa 40% zaidi. Hao ni zaidi ya mashahidi 100,000 na takriban wakimbizi wa ndani milioni 1.9, ambao ni karibu asilimia 90 ya wakaazi wa Ukanda wa Gaza, ambao wanaishi katika mazingira yasiyo ya kibinadamu, na kunyimwa mahitaji ya kimsingi ya maisha. Gaza inakabiliwa na njaa ya kweli, haswa katika sehemu ya kaskazini ya Ukanda huo. Hospitali zinafanya kazi chini ya 30% ya uwezo wao, na uhaba wa dawa na mafuta unaweka makumi ya maelfu ya wagonjwa katika hatari ya kifo cha polepole. Takwimu hizi zinafichua ukubwa wa maafa hayo na kuthibitisha kuwa kinachoendelea ni vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Gaza.

Al-Sisi anasema kuwa kufungua vivuko hivyo kwa nguvu kunamaanisha kuingia katika mzozo na dola kuu, kukataa kualikwa na mtu yeyote kuingia katika mzozo kwa ajili ya watu wa Gaza, kwa madai kuwa hataki kuiburuza Misri na watu wake katika vita vipya! Hata hivyo, kiuhalisia, anaizingira Gaza na watu wake, na kama angeweza, angewanyima hata hewa hiyo wanayopumua. Yeye ni yule yule aliyefuja gesi ya Misri na maji ya Nile, akiifunga kwa mikopo, mikataba, na makubaliano ambayo yataifanya kuwa tegemezi kwa miongo kadhaa ijayo. Hakuna ushahidi wa wazi zaidi wa hili zaidi ya ishara ya serikali yake ya shabaha ya kupunguza deni hadi 55% ifikapo mwaka 2050, bila kujali wazi Misri na watu wake.

Tatizo la kimsingi halipo katika wingi wa misaada na taratibu za kuipeana, bali ni kutokuwepo kwa chombo kimfumo cha kisiasa kinachouongoza Ummah kwa msingi wa Uislamu, kuunganisha nguvu zake, na kutumia uwezo wake kukabiliana na adui yake. Ummah uliishi kwa karne kumi na tatu chini ya Khilafah, na hakuna adui hata mmoja aliyeikalia kimabavu  shubiri hata moja ya ardhi yake bila ya Ummah kuinuka kumfukuza. Leo hii, baada ya kuvunjwa kwa, Palestina imekuwa mateka wa tawala zilizogawanyika na za kitumwa, na watu wake wanalilia msaada pasi na wa kujibu!

Wanazuoni wa Ummah kwa kauli moja walikubaliana kuwa kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa ni faradhi. Amesema Imam Shafi: “Adui akija katika ulimwengu wa Kiislamu, ni wajibu kwa kila mwenye uwezo atoke na kupigana naye.” Ibn Qudamah amesema katika al-Mughni: “Adui akiishambulia nchi, ni faradhi kwa watu wake kumfukuza, na jihad wakati huo inakuwa ni faradhi kwa kila mtu binafsi.” Kwa maana nyengine, kuwalinda watu wa Gaza ni wajibu ambao unahitajika kwa haraka zaidi kwa Ummah mzima, na linalotakiwa kwa haraka zaidi kwa nchi zinazoizunguka, hususan Misri.

Madai ya Al-Sisi kwamba misaada kwa watu wa Gaza inaweza tu kutolewa kwa uratibu pamoja na Mayahudi ni hoja isiyo na maana. Mvamizi anawezaje kuwa hasimu na hakimu wakati huo huo? Shariah hairuhusu kuomba ruhusu kutoka kwa adui wa Ummah kupeleka dawa au chakula kwa watoto wa Kiislamu. Bali, ni wajibu kwamba vivuko na mipaka, kuta, na nyua kati ya Misri na Gaza lazima ziondolewe, na rasilimali za Umma zitumike kuwanusuru watu wa Gaza, na si kutoa uhalali kwa Mayahudi wanaodhibiti mkate na dawa zao.

Enyi wenye ikhlasi katika majeshi ya Ummah kwa jumla na hasa jeshi la Misri: Damu ya watoto wa Gaza, heshima ya wanawake wake, na mabaki ya miili ya wanaume wake ni amana juu ya shingo zenu. Mwenyezi Mungu atakuulizeni Siku ya Kiyama: Je! Mlifanya nini ili kuwanusuru kaka na dada zenu? Hamuna udhuru wa kuwa na mamlaka na vifaa na kisha kuviacha vikifungiwa huku kaka na dada zenu wakililia msaada na nusra. Ni wajibu wenu kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu na kusimama pamoja na Ummah wenu. Kateni pingu mulizofungwa nazo na wakoloni na tumieni silaha zenu mahali zinapostahili: dhidi ya adui wa Mwenyezi Mungu na adui yenu. Jueni kuwa Ummah uko pamoja nanyi, na kwamba Mwenyezi Mungu atakunusuruni ikiwa nyinyi ni wakweli kwake.

[إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.