Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  9 Rabi' II 1447 Na: 1447 / 09
M.  Jumatano, 01 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mpango wa Trump ni Uvamizi wa Kikatili wa Kijeshi Ambao Unahitaji Haraka Kubadilishwa kwa Watawala Wanaokubaliana na Mpango Wake
(Imetafsiriwa)

Katikati ya miaka miwili ya vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendelea mjini Gaza, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza mpango wa kina unaolenga kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza na kufikia “amani ya kudumu” katika Mashariki ya Kati. Mpango huu ulitangazwa wakati wa mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari uliofanyika mnamo Jumatatu, 29/9/2025, na mhalifu aliyelaaniwa Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House. Alisema, “Leo tunalifanyia kazi suluhisho la kina kwa kadhia ya Palestina, sio Gaza pekee.” Miongoni mwa mambo muhimu zaidi katika mpango wake ni mpango wa “kuanzisha chombo kipya cha kimataifa cha uangalizi wa Ukanda wa Gaza kinachoitwa Baraza la Amani.” Aliongeza, “Mimi binafsi nitakuwa mwenyekiti wa baraza hili huko Gaza, kwa ushiriki wa Tony Blair.” Alisisitiza kwamba “washirika wetu wa Kiarabu na Waislamu wako tayari kuchukua majukumu yao kwa Gaza,” na kwamba “ufadhili ni muhimu ili kuruhusu mafanikio mjini Gaza, na tutajenga mustakabali salama zaidi kwa wote.”

Hapo jana, mawaziri wa mambo ya nje wa Qatar, Jordan, Imarati, Indonesia, Pakistan, Uturuki, Saudi Arabia na Misri walitoa taarifa ya pamoja kukaribisha juhudi za dhati za Trump za kumaliza vita huko Gaza. Walithibitisha utayarifu wao wa kushirikiana vyema na kiujenzi pamoja na Marekani na pande husika ili kukamilisha makubaliano hayo na kuhakikisha utekelezaji wake. Walithibitisha imani yao katika uwezo wake wa kutafuta njia ya amani, na katika muktadha huu, walikaribisha tangazo la Trump la pendekezo lake, ambalo linajumuisha kumaliza vita.

Mpango huu wa Trump ni moja tu ya miradi ya kikoloni ambayo kwayo Amerika inataka kulimakinisha umbile la Kiyahudi katika eneo hili na kuifilisi kadhia ya Palestina, kama ilivyokuwa miradi yote ya hapo awali iliyopendekezwa na Wakoloni wa Magharibi kutatua suala la Palestina. Tofauti tu ikiwa ni upanuzi wa umbile la Kiyahudi katika miongo kadhaa, na uvamizi unaoendelea, mauaji, uharibifu na uhamishaji wa watu wa Palestina. Usaliti wa watawala na kile kinachoitwa suluhisho la dola mbili hutukuza utambuzi wa umbile la Kiyahudi na kuhifadhi usalama na uthabiti wake. Ama kuhusu mazungumzo ya kimataifa ya dola ya Palestina, ambayo Netanyahu anayapinga, yamekuwa sio zaidi ya uhuru potofu.

Ama watawala wa Waislamu, hususan wale Trump aliokutana nao na kuwasifu kwa ushirikiano wao katika kutekeleza mpango wake huo, wamezoea udhalili na usaliti. Hao ndio waliowaangusha watu wa Gaza na wakakataa kuwanusuru. Hao ndio waliojitwika jukumu la kujinasibisha na Marekani na umbile la Kiyahudi katika kulitiisha eneo hili na kuzitiisha nchi zake, watu na majeshi yake kwa ajili ya kuwatumikia maadui wa Umma waliolaaniwa sana.

Mkutano wa Mfalme na mawaziri wakuu wa zamani baada ya kuregea kutoka kukutana na Trump haukuwa na nia ya kuepusha tishio linaloikabili Jordan. Haukuwa mkutano wa mashauriano au uwazi, bali ni agizo kwao kuendelea na kile alichokitaja kuwa makubaliano ya pamoja juu ya mpango wa Trump. Hii inaakisi upingaji wa kweli wa watu wa Jordan kwa masuluhisho ya kusalim amri ya Amerika, yaliyoonyeshwa kupitia maandamano ya mabarabarani na operesheni za kishujaa.

Mtazamo wenye utambuzi juu ya yale ambayo Umma wa Kiislamu umekabiliana nayo katika vijidola vya kitaifa vilivyoundwa na mkoloni kafiri Magharibi kutokana na kukaliwa kimabavu, kuua, kuhamishwa, uporaji, udhalilishaji, na juu ya yote, kutengwa kwa hukmu ya Uislamu na kumuasi Mwenyezi Mungu (swt) kunatokana na kutokuwepo kwa dola ya Kiislamu, ambayo Khalifa wake alikuwa ngao na watu kupigana nyuma yake. Hii ndiyo hali ambayo Waislamu wanapaswa kuifanya suala lao la kwanza kabisa na nyeti, ambalo litaregesha fahari yao, heshima, utawala juu ya ardhi zao na utashi wao.

Masuluhisho ambayo Amerika inaweka mbele kwa ile knayoitwa Mashariki ya Kati yanakataliwa kwa jumla, kwa sababu inataka kuidhibiti Palestina na nchi zote za Kiislamu, ikiongezewa na uharamu wake uliothibitishwa. Madai ya waliokatishwa tamaa na waliodanganyika kwamba hatuna uwezo wa kukabiliana na Marekani na chombo chake, umbile la Kiyahudi, hayana msingi katika ukweli.

[أَلَيْسَ اللَّهُ بِكَافٍ عَبْدَهُ وَيُخَوِّفُونَكَ بِالَّذِينَ مِن دُونِهِ وَمَن يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ]

Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasio kuwa Yeye! Na aliye hukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea hana wa kumwongoa. [Az-Zumar: 36]

Marekani na Mayahudi wameshindwa kuishinda Gaza, ambayo inapigana peke yake. Uhalisia ambao lazima ueleweke ni kwamba suluhisho lipo katika kuwaondoa watawala walio chini yao na kusimamisha dola moja ya Kiislamu kwenye magofu ya viti vyao vya enzi. Kitu chengine chochote kando na hili ni kazi bure, kuondoka kwenye suluhisho la Shariah, na kurefusha mateso ya Umma wa Kiislamu, kwani ndilo suala kuu ambalo ni ufunguo wa suluhisho la ushindi na tamkini ambao Mwenyezi Mungu (swt) ameahidi kuufikia.

[الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَاناً وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ]

Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa. [Aal-i-Imran: 173]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.