Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  5 Rabi' I 1448 Na: Afg. 1448 H / 03
M.  Jumanne, 18 Agosti 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Balozi za Marekani ni Vituo vya Ujasusi na Ugomvi; Kuialika Marekani Kufungua Ubalozi Wake Tena nchini Afghanistan ni Usaliti kwa Mihanga ya Ummah wa Kiislamu na Tusi kwa Damu ya Mashahidi

(Imetafsiriwa)

Katika mahojiano ya hivi karibuni na The New York Times jijini Kabul, waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan aliialika rasmi Marekani kufungua tena ubalozi wake na kuwekeza katika sekta za miundombinu na madini za Afghanistan, akisema: "Tunachukulia sura ya vita kuwa imefikia mwisho, na kuanzia sasa, tunataka uhusiano unaotegemea heshima ya pande zote na mwanzo wa sura mpya ya ushirikiano chanya."

Kuzungumzia "mwisho wa sura ya vita" na dola ambayo inashiriki katika vita vipana na vya uadui dhidi ya Ummah wa Kiislamu ni kosa la kimkakati na kitendo cha kufumbia macho ukweli usiopingika. Marekani ni kiongozi wa ukafiri wa kimataifa na adui mkuu wa Waislamu. Ingawa Marekani kwa sasa haipigani vita vya kijeshi nchini Afghanistan, mtazamo unaozingatia Ummah unaweka wazi kwamba Amerika, kwa wakati huu, inapigana na Waislamu katika nyanja kadhaa na iko mstari wa mbele katika migogoro hiyo. Marekani inacheza dori katika vita vya Yemen na mgogoro wa umwagaji damu nchini Sudan; inawapa Mayahudi msaada usio na kikomo wa kijeshi, kisiasa, na silaha katika mauaji ya halaiki ya watu wa Palestina na Lebanon; Pia imefuata sera za shinikizo, vikwazo, na mapambano dhidi ya Iran. Pamoja na maendeleo haya, inaunga mkono sera za serikali ya India za uvamizi na ukandamizaji dhidi ya Waislamu, kuongezeka kwa taharuki na Pakistan dhidi ya Afghanistan, na kuwekwa kwa mashinikizo la kisiasa, kiuchumi, na usalama dhidi ya Afghanistan.

Katika mizani ya Uislamu, kipimo cha al-walāʾ wa al-barāʾ hakiamuliwi na mipaka ya kikoloni au fahamu za kitaifa. Uadui dhidi ya Marekani umejikita katika mapambano ya kimsingi kati ya ukafiri na Uislamu. Kupuuza uhalifu wa dola hii ya kikoloni katika ardhi za Waislamu kwa kisingizio cha maslahi ya kitaifa ni kuondoka kutoka kwa kanuni za imani ya Kiislamu na kupuuza mtazamo mmoja wa kisiasa wa Uislamu. Zaidi ya hayo, uadui wa Amerika dhidi ya Afghanistan haujawahi kuisha. Kutokuwepo uwepo wa kijeshi wa Marekani hakumaanishi kwamba vita vimekwisha au kwamba amani imeanzishwa; badala yake, Marekani imebadilisha mbinu yake kutoka vita vya moja kwa moja vya kijeshi hadi shinikizo la kiuchumi na kisiasa na operesheni za kijasusi. Kufungiwa na kukamatwa kwa mabilioni ya dolari katika akiba ya benki kuu, kuwekwa kwa vikwazo vya kiuchumi, ukiukwaji wa uhuru wa anga ya Afghanistan, na kampeni kubwa ya propaganda dhidi ya maadili ya Kiislamu yote yanaendelea kwa nguvu zote. Kwa hivyo, kutoka kwa mtazamo wa kisheria wa Kiislamu, kuanzisha uhusiano wowote wa kidiplomasia, kisiasa, au kiuchumi na "dola yenye uhasama” ambayo mikono yake imejaa damu ya Waislamu ni batili na ni haramu.

Kwa upande mwengine, kuyaalika makampuni ya Marekani na serikali ya Marekani kuchimba madini ya Afghanistan na kupata udhibiti wa miundombinu yake kunaleta maafa mawili.

Kwanza, dola za kibepari za Magharibi zimekuwa zikiziona ardhi dhaifu kama mawindo ya kuporwa. Sera hii ya uwindaji ilidhihirishwa kikamilifu katika makubaliano ya hivi karibuni kuhusu Ukraine, ambapo msaada wa Marekani ulihusishwa na kupata udhibiti na usimamizi wa rasilimali za madini, mafuta, na gesi, na hivyo kupelekea aina ya "kukamatwa kwa mali ya mtindo wa kikoloni."

Pili, madini na maliasili za ardhi za Waislamu ni mali ya Ummah na lazima zitumike kwa maslahi na nguvu ya Waislamu na kwa ajili ya kudhihirisha Dini. Kwa kuwa madini ya kimkakati yana dori muhimu katika viwanda vya makombora, mifumo ya rada, na teknolojia za ulinzi na kijeshi, kukabidhi rasilimali hizi muhimu ni sawa na kusaidia kudumisha nguvu ya kikoloni ya Amerika, kudhoofisha Waislamu, na kuimarisha upanga wa adui anayezitumia kutengeneza makombora na mabomu ambayo kisha huangushwa juu ya watu waliokandamizwa wa Gaza, Lebanon, na nchi zengine za Kiislamu.

Waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan pia alikuwa amesema hapo awali kwamba: "Ninaamini uwezo wa Rais Trump wa kufanya mikataba, mbinu yake ya kivitendo, na uamuzi wake ni mambo ambayo yanaweza kuwezesha ushirikiano mzuri na utawala wake." Dhana kama hiyo kuhusu wanasiasa wa Marekani, haswa Donald Trump, inagongana kabisa na mtazamo wa Kiislamu. Mtazamo wa Trump kuhusu ulimwengu ni wa umiliki na wa kikoloni. Anaendelea kuwa na matarajio ya kuchukua udhibiti wa Kambi ya Anga ya Bagram, anaunga mkono unyakuzi kamili wa Palestina, na sasa anazungumzia kwa ukali kutangaza Mlango-Bahari wa Hormuz kuwa sehemu ya eneo la Marekani.

Je, unasisitiza kuendelea kushirikiana kwa karibu na mtu ambaye sio tu anaupiga vita Uislamu kivitendo, lakini pia anatangaza uadui wake waziwazi kwa maneno pia? Wakati wa muhula wake wa kwanza wa urais, Trump alitangaza waziwazi: "Tutaunganisha ulimwengu uliostaarabika dhidi ya ugaidi mkali wa Kiislamu, ambao tutauondoa kabisa kutoka kwenye uso wa Dunia."

Kwa hivyo, badala ya kuweka matumaini yako katika dola za kikoloni za Magharibi na kuingia katika mikataba nazo, nyoosheni mkono wa udugu kwa Waislamu—marafiki zenu wa kweli—wanaowaita kuelekea chanzo cha heshima ya kweli: kusimamishwa upya kwa Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume. Wito huu wa kweli, tofauti na siasa za vitendo za Magharibi, sio muamala wa kibiashara au kiuchumi; badala yake, ni muamala mtukufu na Mwenyezi Mungu (swt). Kutoa nusra kwa dawah hii kutakuongozeni kwenye heshima, nguvu, na nafasi ya uongozi duniani, kama vile Uislamu ulivyowahi kuwainua Waarabu waliogawanyika na waliokuwa wajinga kutoka pembezoni mwa historia hadi nafasi ya uongozi na amri ulimwenguni.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُوا لِلَّهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu?” [Surah An-Nisa: 144]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.