Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  30 Rabi' I 1447 Na: H 1447 / 05
M.  Jumatatu, 22 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kiburi cha Trump Lazima Kijibiwe kwa Kusimamisha Tena Khilafah Rashida ya Pili!
(Imetafsiriwa)

Kwa mara nyengine tena, Donald Trump amechukua msimamo wa kiburi na vitisho kuelekea serikali ya Afghanistan na Waislamu, na kutangaza: “Ikiwa Afghanistan haitarudisha Kambi ya Anga ya Bagram kwa wale walioijenga, Marekani, MAMBO MABAYA YATATOKEA,”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inalaani matamshi ya Trump kwa maneno makali iwezekanavyo. Inachukulia makubaliano yoyote juu ya jambo hili kama usaliti kwa Uislamu, jihadi, na sababu ya mashahidi, na inaonya kwamba uwepo wowote mpya wa Waamerika – jina lolote itakalochukua – utaigeuza Afghanistan kuwa uwanja wa vita vya ushindani wa dola kubwa na za kikoloni.

Matamshi ya Trump yanaweza kusomwa kama jaribio la kushinikiza mamlaka za Afghanistan kupata makubaliano ya kisiasa, kiuchumi, au usalama, au kama tishio linaloelekezwa kwa dola za kikanda. Kilicho wazi, hata hivyo, ni mtazamo wake wa kibeberu, ukaliaji kimabavu kwa Afghanistan. Kambi ya anga ya Bagram, ambayo zamani ilikuwa kituo cha makumi ya maelfu ya wanajeshi wa Marekani na ishara ya nguvu ya Amerika katika eneo hilo, ilihamishwa kufuatia kushindwa kwa Amerika katika vita vya Afghanistan. Kujiondoa kwa Marekani kutoka Bagram haikuwa tu mwisho wa uwepo wa kijeshi; pia ilikuwa ishara ya kupungua kwa nguvu na ushawishi wa Amerika kikanda na kimataifa – kushindwa ambayo sasa kunamtafuna Trump.

Wakati huo huo, baadhi ya watu wa ndani na nje wanajaribu, kupitia ushirikiano au shinikizo la kisiasa, kubadilisha baadhi ya vipimo vya Kiislamu vya watawala na kuwashawishi kukubali, kuafikiana, au kufanya mikataba kuhusu suala hili. Wale wanaofikiria kuwa ushirikiano wa karibu na Marekani, au hata kurudi kijeshi kungenufaisha Afghanistan wamekosea sana. Huu ni udanganyifu ule ule uliowafanya watawala wa khiyana wa Kiarabu kuipa makaazi Marekani, na hoja hiyo hiyo ambayo watawala wa republican walitoa, mantiki ambayo haikuzaa chochote isipokuwa udhalilifu, kukimbia, kuanguka, na kujiweka mbali na Uislamu.

Ardhi za Kiislamu ni za Waislamu, na sheria ya Kiislamu (shariʿa) pekee ndiyo yenye mamlaka halali ya kuamua hatima yao. Marekani – dola yenye uhasama – haisimama tu katika upinzani wa kimfumo na kisiasa bali katika uadui wa kijeshi dhidi ya Umma wa Kiislamu na, kwa hakika, dhidi ya wanadamu. Marekani imeunga mkono waziwazi mauaji ya halaiki ya Gaza yanayotekelezwa na serikali ya Kizayuni na hivi sasa inatayarisha uuzaji wa silaha kwa ‘Israel’ wenye thamani ya dolari za Kimarekani bilioni 6.4 ili Waislamu wengi zaidi wauawe, wahamishwe makwao na kuangamizwa kwa njaa. Je, Uislamu unatoa jibu gani kwa madhalimu wenye kiburi kama hao isipokuwa jihad na mapambano ya silaha?

Watawala wa Afghanistan wanapaswa kuelewa kwamba Ibtila (jaribio) hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ili kuwatenganisha wenye kushukuru na wasio na shukrani. Lazima wafanye kazi ili kuweka roho ya Uislamu, uthabiti, na jihad hai katika jamii kwa njia ya kimfumo. Ni lazima wajihadhari na udhalilifu na mapenzi ya dunia hii kwao wenyewe na kwa jamii. Kama alivyosema Mtume (saw) alipoulizwa ni wahn (udhaifu) ni nini?

وَمَا الْوَهْنُ؟ قَالَ: «حُبُّ الدُّنْيَا وَكَرَاهِيَةُ الْمَوْتِ»

Akajibu: “Kuipenda dunia, na kuchukia kifo” – sifa hizi humfanya adui aache kuwaogopa Waislamu. Ijapokuwa Trump anatishia na kutaka kuutisha mfumo unaotawala kwa matokeo, lazima tukumbuke kwamba Shetani pia ananong'ona na kueneza hofu kuhusu matokeo ya matendo fulani; hatupaswi kuruhusu matamshi kama hayo ya kishetani, ya kiburi yajaze nyoyo zetu hofu au kutusukuma kusalimu amri. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّمَا ذَلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ]

“Hakika huyo ni Shet'ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.” [Aal-i ʿImran 3:175].

Kumbukeni: maadamu tu tunaendelea kufungiwa ndani ya muundo wa kisasa wa dola za kitaifa na vipimo vyake vya sasa vya kisiasa, roho yetu ya jihad itadhoofika; katika kutafuta ukaribu na mfumo wa kimataifa tunahatarisha kurudia historia ya ukoloni nchini Afghanistan. Maadui wanaendelea kutumia uhadaifu, hila na kupanga kuwadhoofisha Waislamu. Kwa hiyo, mpaka tutakapounda nguzo ya kisiasa iliyoegemezwa juu ya Uislamu na Umma wa Kiislamu – na mpaka tutakaposimamisha tena Khilafah Rashida – adui ataendelea kututishia waziwazi na kuzungumza juu ya kuzikalia kimabavu ardhi zetu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.