Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kukipokonya Silaha Chama cha Iran na Dori ya Mamlaka ya Lebanon!
(Imetafsiriwa)

Makubaliano ya kusitisha mapigano ya tarehe 27/11/2024, kati ya umbile la Kiyahudi na mamlaka za Lebanon, chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Marekani, yaliweka msingi wa kisiasa wa kukipokonya silaha chama cha Iran na mirengo mengine ya Palestina nchini Lebanon. Hii haikuwa kutokana na kutaka "amani" kutoka Marekani, bali ni kuhakikisha usalama wa umbile la Kiyahudi katika maandalizi ya kuondoa uwezo mdogo uliobaki wa Waislamu wa kupigana nao, hasa baada ya matukio ya Kimbunga cha Al-Aqsa. Makubaliano haya ni sehemu ya mpango wa kimkakati wa usalama unaoongozwa na Amerika kuweka upya sauti ya eneo hilo kwa njia inayolingana na maslahi yake katika kipindi kijacho. Kama ambavyo uhalisia umekuwa sambamba na maslahi yake katika miaka ya hivi karibuni. Kwa hakika, ni karata ya Marekani ambayo lazima itekelezwe na upande wa Lebanon, kama ilivyoelezwa katika taarifa ya Rais kwa Al-Hadath TV mnamo tarehe 8/8/2025, aliposema: “Kutekeleza karata ya Marekani kunahitaji idhini ya Syria na ‘Israel’ kwa dhamana ya Marekani na Ufaransa”!

Karata hii ya Marekani inabainisha, kama ilivyoelezwa wazi na mjumbe wa Marekani Tom Barrack, kwamba Hizb (chama) cha Iran ambacho kimetumikia kwa muda mrefu sera ya Iran inayozunguka duara la Amerika nchini Lebanon, Syria, na kwengineko, kitaajiriwa tena ndani ya mizani ya madaraka kwa kukibadilisha kuwa chama cha kisiasa na kukipokonya silaha zake nzito. Hili ni kwa mujibu wa maslahi ya kikanda ya Amerika na dira yake kwa eneo ambalo limeegemezwa juu ya kulihifadhi umbile la Kiyahudi mpaka mahusiano nalo yahalalishwe, kuliunganisha, na kuwa nao katika eneo hilo kana kwamba ni chombo cha kimaumbile na sio mkaliaji kimabavu wa ardhi ya Kiislamu, ambapo haki za Waislamu hazitapokonywa, haijalishi ni muda kiasi gani unapita, ni muda kiasi gani uvamizi huo utadumu, au iwapo dola kuu au watawala vibaraka katika nchi za Kiislamu watalikubali.

Yeyote atakayechunguza makubaliano ya usitishaji mapigano ataona kwamba hayakuweka bayana kuhusu kupokonywa silaha mara moja kwa chama cha Iran nchini Lebanon, bali yalijumuisha vifungu vilivyofungua njia kwa hili hatua kwa hatua, ikiwa ni pamoja na kutengwa kwa silaha mikononi mwa dola ya Lebanon kusini mwa Mto Litani. Yeyote anayechunguza kile kinachotokea kwa kuitishwa kwa kikao cha baraza la mawaziri kujadili kutengwa kwa silaha mikononi mwa serikali baada ya zaidi ya miezi minane, na ukiukaji wa umbile hilo wa masharti ya makubaliano katika suala la kutojiondoa kutoka sehemu zote kusini mwa Mto Litani, pamoja na kufanya mashambulizi dhidi ya watu katika eneo lote la Lebanon ... ataona kuwa Mayahudi kimsingi wanataka kuleta hali ya mgawanyiko wa kisiasa na kusababisha mgawanyiko wa ndani wa Lebanon katika ya makundi ya kisiasa nchini Lebanon, na kupelekea mizozo kati ya vipengee vya watu wake.

Kwa hiyo, ni lazima iwe wazi kwa watu wa Lebanon kwa jumla, na hasa Waislamu:

1- Suala la Waislamu kwa jumla kumiliki silaha za kupigana na umbile la Kiyahudi ni suala la Kiislamu zaidi ya yote. Hukmu juu yake inategemea Uislamu pekee, sio Amerika, Mayahudi, au sheria za kimataifa zinazowakilishwa na Umoja tasa wa Mataifa. Mazingatio ya kimadhehebu au ya kimakundi hayapaswi kamwe kuingilia kati.

2- Ni wajibu wa Ummah kuwakusanya wanawe kutoka kwa watu wenye nguvu ili kutimiza wajibu wao wa kuikomboa ardhi kutokana na uchafu wa Mayahudi na kukomesha mauaji yao ya Waislamu. Matumizi yoyote ya silaha nje ya mfumo huu, hasa yanapoelekezwa dhidi ya Waislamu, kama yalivyotokea nchini Lebanon na Syria, ni haramu kwa Waislamu kujihusisha nayo, na ni usaliti kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, Dini Yake, na Waislamu.

3- Iwapo watawala wa nchi za Kiislamu hawataruhusu majeshi kusonga ili kuwakomboa Waislamu wa Gaza na Palestina kutokana na jinai wanazoteseka, basi inakuwa ni wajibu wa majeshi kushirikiana na wale wanaotaka kusimamishwa Dola ya Khilafah kutoka kwa wana wa Hizb ut Tahrir wanaotokana nao na miongoni mwao, na kuwanusuru. Huu ndio wajibu wa zama hizi. Kwa sababu imedhihirika kwamba hakuna atakayekabiliana na janga hili la jumla isipokuwa Dola ya Khilafah, ambayo ndiyo itakayolikomesha umbile la Kiyahudi na kukata kamba zinazolipatia nguvu, dhulma na uhalifu. Inaonekana kana kwamba Mwenyezi Mungu (swt) anaitengeneza njia ya kuisimamisha ili iweze kutekeleza dori hii kubwa, na kupitia hilo, Mwenyezi Mungu atatimiza bishara njema za Mtume Wake (saw): Al-Bukhari na Muslim wamesimulia katika Sahih zao kutoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حتَّى تُقاتِلُوا اليَهُودَ، حتَّى يَقُولَ الحَجَرُ وراءَهُ اليَهُودِيُّ: يا مُسْلِمُ، هذا يَهُودِيٌّ وَرَائِي فَاقْتُلْهُ» “Hakitasimama Kiyama mpaka mupigane na Mayahudi mpaka jiwe ambalo amesimama Yahudi nyuma yake liseme: Ewe Muislamu, huyu hapa Yahudi nyuma yangu, basi muuwe.

4- Katika dhurufu hizi, haijuzu kwa Waislamu kuingia katika hali ya amani na Mayahudi hasa katika wakati ambapo wanafanya ukatili wa kinyama na wa kutisha dhidi ya Waislamu, na mandhari ya Gaza bado ni mbichi katika fikra za kila mtu... Kwa hakika, kunaweza kuwa na tafsiri moja tu ya hili: kwamba itapelekea tu kwenye amani ya wale “walioshinda” na kulazimishiwa masharti Waislamu waliokubali kushindwa.

5- Walichokifanya wawili hao na chama cha Iran katika kujibu uamuzi wa serikali wa kuzuia umiliki wa silaha kwa dola, kwa kupeperusha mantiki ya nguvu na kutumia barabara mara kwa mara na kwa njia isiyokubalika, bila kuchukua hatua za kweli za kisiasa, kama vile kuondoka serikalini, kwa mfano, au kujiuzulu kwa wawakilishi wa wawili hao! Hii inaonyesha kuwa hali hiyo haihusiani kabisa na silaha, lakini inaingia katika mzunguko wa majadiliano na mazungumzo juu ya mafanikio ya mamlaka katika kipindi kijacho. Hili ni jambo ambalo Walebanon wote wanapaswa kufahamu, wasije wakawa wahanga wa manufaa ya madaraka yanayotafutwa na chama kimoja au chengine, katika ulingo wa kisiasa ambao umekuwa ukijirudia na kuchosha tangu 2005.

6- Wale wanaokubali kujiita "walio wachache" lazima wawe upande wa Waislamu na wasimame nao katika mambo yao, na wasiburuzwe kwenye safu za maadui zao. Uislamu umewaheshimu kwa kuwafanya raia wa dola ya Kiislamu (wana haki sawa na Waislamu, na wanastahiki uadilifu sawa na Waislamu). Uislamu haujakubali kuwaita "walio wachache" kama nchi za Magharibi zilivyowaita. Wanapaswa kujua kwamba kama watakataa kuchukua upande wowote, watahukumiwa kama mtu yeyote ambaye wanatafuta msaada kutoka kwake dhidi ya Ummah.

Hatimaye, tunatoa wito kwa Waislamu nchini Lebanon kukataa kila njama zinazolenga kuliimarisha umbile nyakuzi la Kiyahudi, kufilisi nishati iliyobaki ya Ummah, na kuziba njia yao ya kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu katika dola ya Khilafah kwa njia ya Utume. Wanapaswa kuwa na yakini kwamba uhalisia huu mchungu hautatatuliwa katika vipengee vyake vyote isipokuwa kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itaunganisha ardhi za Waislamu na kuwakomboa waliokaliwa kimabavu kutokana nao. Kwa hiyo, mnakaribishwa kufanya kazi nasi katika kusimamisha Khilafah ambayo itakusanya silaha tena chini ya bendera moja: bendera ya “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu,” na kauli mbiu “Na waandalieni nguvu kadri muwezazo,” kwani Khilafah inakuja bila shaka, kwa kuwa ni hatua ya mwisho katika hatua za kisiasa za Ummah baada ya utawala wa kidhalimu, ambao ulielezwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika Hadith:

«تكونُ النُّبُوَّةُ فيكم ما شاء اللهُ أن تكونَ، ثم يَرْفَعُها اللهُ تعالى، ثم تكونُ خلافةٌ على مِنهاجِ النُّبُوَّةِ ما شاء اللهُ أن تكونَ، ثم يَرْفَعُها اللهُ تعالى، ثم تكونُ مُلْكاً عاضّاً، فتكونُ ما شاء اللهُ أن تكونَ، ثم يَرْفَعُها اللهُ تعالى، ثم تكونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فيكونُ ما شاء اللهُ أن يكونَ، ثم يَرْفَعُها اللهُ تعالى، ثم تكونُ خلافةً على مِنهاجِ نُبُوَّةٍ» ثم سكت ﷺ

“Utume utadumu kwenu kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha ataunyanyua, kisha itakuja Khilafah kwa njia ya Utume, na itadumu kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha atainyanyua, kisha kutakuwa na utawala wa kurithi (ملكًا عاضًا), na utakaa hapo kwa muda utakao Mwenyezi Mungu kisha ataunyanyua, kisha kutakuwa na utawala wa kidhalimu (ملكًا جبرية), na utadumu kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha Ataunyanyua. Kisha itakuwa Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha (saw) akanyamaza”.

Basi kuweni miongoni mwa askari na mashahidi wake, na musiwe miongoni mwa zana za maadui zake.

H. 16 Safar 1447
M. : Jumapili, 10 Agosti 2025

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.