Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali

Hati ya Mkakati wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani
(Imetafsiriwa)

Swali:

Mnamo tarehe 5/12/2025, Trump alitangaza kwa umma hati mpya ya Mkakati wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani yenye kurasa 33. Kuna tofauti gani kati ya hati hii na zile zilizotangulia, kama vile mkakati wa Biden?

Jibu:

Uchunguzi wa makini wa hati hizi hauonyeshi tofauti yoyote ya msingi kati ya hati za Mkakati wa Usalama wa Taifa zilizochapishwa na Trump wa Republican mnamo 2017 na 2025, au zile zilizochapishwa na Reagan mnamo 1988, Bush Baba mnamo 1990, na Bush Mwana mnamo 2002, na zile zilizotangazwa na marais wa Democratic: Clinton mnamo 1994 na 1998, Obama mnamo 2010 na 2015, na Biden mnamo 2022. Tofauti pekee iko katika mtindo na lugha inayotumika; zote zinalenga kudumisha na kuimarisha udhibiti wa kimataifa wa Marekani. Ingawa Wanarepublican wanaelezea uongozi wa kimataifa wa Marekani kwa uwazi na bila utata, Wanademocrat hutumia lugha ya maua na ya udanganyifu, wakati mwingine kupitia kupotosha na nyakati zengine kupitia kauli ngumu na zisizoeleweka. Katika jibu langu, kama swali linavyoashiria, nitazingatia tofauti kati ya mikakati hii badala ya kuzama ndani ya maelezo yake, isipokuwa kwa kiwango kinachohitajika ili kufafanua tofauti kati ya mkakati wa Biden na mkakati wa Trump. Ili kuonyesha hili, na kwa muongozo wa Mwenyezi Mungu, nasema:

1- Jibu la Swali tulilotoa mnamo 18/11/2016, lilisema yafuatayo:

(…Umbo la siasa za Marekani halitofautiani kati ya Chama cha Republican na Chama cha Democratic, lakini mitindo ndio hutofautiana. Sababu ya hili inahusishwa na historia ya kuibuka kwa vyama hivyo viwili. Chama cha Republican hakijali sana kuonekana katika hisia za kidemokrasia kwamba wanazungumza kwa sauti kubwa, lakini kinatawaliwa na mtazamo wa cowboy uliojaa kiburi na umeibuka kutoka katika mazingira haya na bado kinauendeleza... Na utamaduni wa cowboy huelekea kwa mtu anayeonyesha nguvu, kumpiga na kumuua mwengine, kupuliza hapa na pale… Wala hawajali kuhusu uhalifu wa kuua watu wasio na hatia, kwani umeenea katika nchi yao, na wanapenda kubeba silaha na kuzitumia kama matamanio. Bunge la Seneti la Marekani lilikataa mnamo Jumatatu pendekezo la Chama cha Democratic ambalo linaruhusu uchunguzi unaopanuka wa historia ya jinai na kisaikolojia kwa wale wanaopenda kununua silaha za kibinafsi... Kwa hivyo, Wanarepublican hawajali kuhusu udhibiti wa umiliki wa bunduki kwa sababu ya udhibiti wa wazalishaji na wafanyibiashara wa silaha kuwashawishi wao…Ilhali, Chama cha Kidemokrasia kinatawaliwa na udanganyifu, kikionekana katika hisia za uongo za kidemokrasia na kuiga mtindo wa Kiingereza. Kinatoa sumu iliyofinikwa na mafuta bandia, na kukuua kwa tabasamu, huku chama cha Republican kikitoa sumu safi, kwa hivyo kinakuua huku kikiuma meno yake... Kwa hivyo, marais wa Kidemokrasia wana uwezo zaidi wa kudanganya na kujishinda imani ya wanaowadanga, ilhali marais wa Republican hawadanganyi mtu yeyote kwa sababu uadui wao unatangazwa waziwazi. Hii inaweza kuonekana wakati wa kuhakiki maono ya watu ya mifano ya historia isiyo mbali sana ya Marais wa pande zote mbili… Bush anatamka kupitia vita vya msalaba huku Obama akinukuu aya ya Quran jijini Cairo... na wote wawili wanapanga mpango dhidi ya Uislamu...! Hiyo ni kama tulivyosema hapo awali: “Kwa hivyo marais wa Kidemokrasia wana uwezo zaidi wa kudanganya na kujishindia imani ya wanaowadanga, ilhali marais wa Republican hawadanganyi mtu yeyote kwa sababu uadui wao unatangazwa waziwazi.”

Hata katika nembo ya pande hizo mbili, kuna tofauti katika maana, inakubaliana na kile tulichosema. Kwa kuwa mchoraji katuni wa Marekani – wenye asili ya Ujerumani – Thomas Nast mnamo (1870 na 1874), alichapisha Mchoro katika Jarida la Harper unaoonyesha picha ya punda akiwa amevaa mwili wa simba ili kuwatisha kundi la wanyama, miongoni mwao ndovu mkubwa wa porini anayeharibu mazingira yake... Tangu wakati huo, punda amekuwa nembo ya chama cha Democratic, na ndovu huyo akawa nembo ya chama cha Republican, na nembo hizo mbili zinaonyesha taswira ya vyama hivyo viwili... Kwa hivyo, vitendo vya Trump si uvumbuzi mpya wa vitendo vya wagombea wa Republican, isipokuwa kwa kiwango cha sifa za kibinafsi zinazomtofautisha mtu kwa mwengine, lakini sifa za jumla za Chama cha Republican zinabaki kuwa karibu zinazotumika kwa wagombea wote wa chama isipokuwa sifa za kibinafsi kama ilivyotajwa hapo juu.) Mwisho wa Nukuu.

2- Kwa hivyo, kiburi cha asili cha Wanarepublican na mbinu za udanganyifu za Wanademocrat zinaonekana wazi katika hati za kimkakati zilizotangazwa na marais kutoka pande zote mbili.

* Mkakati wa Biden, kwa mfano, unatafuta kuendeleza uongozi wa Marekani na kuimarisha utawala na utaratibu wa kimataifa kupitia misamiati ya kupotosha kama vile ushirikiano, demokrasia, haki za binadamu, na diplomasia.

* Ama kuhusu Trump, ambaye shakhsiya wake ina sifa ya kiburi kupita kiasi, tamaa ya madaraka, kupenda kujionyesha, ukosefu wa hekima, mwelekeo wa mizozo ya ndani na kuwamaliza wapinzani, na hali ya wimbi la kuzuzua, analenga kudumisha uongozi wa kimataifa wa Marekani kupitia kaulimbiu zilizo wazi na zisizofichwa kama vile “Amerika Kwanza” na “Amani Kupitia Nguvu,” hata kufikia hatua ya kuwatukana washirika wake bila udhuru wowote. Hivi ndivyo Trump alivyosema waziwazi katika hati yake ya kimkakati: (“Lengo la mkakati huu ni kuunganisha pamoja mali hizi zote zinazoongoza duniani, na nyenginezo, ili kuimarisha nguvu ya Amerika na ukuu na kuifanya nchi yetu iwe tukufu zaidi kuliko ilivyo wahi kuwa.” (National Security Strategy 2025, https://www.whitehouse.gov/wp-content/uploads/2025/12/2025-National-Security-Strategy.pdf)).

Zaidi ya hayo, katika karibu vichwa vidogo vyote chini ya kichwa kikuu “Vipaumbele,” ulinzi, uimarishaji, na uendelevu wa udhibiti wa Marekani vinasisitizwa na kuimarishwa. Hizi ni pamoja na: Upangiliaji upya kupitia amani, usalama wa kiuchumi, Mizani ya biashara ya ndani na nje, kupata mwanya kwenye silsila muhimu za usambazaji na nyezo, kufufua msingi wetu wa viwanda vya ulinzi, udhibiti wa nishati, na kuhifadhi na kukuza udhibiti wa sekta ya fedha ya Marekani.

3- Hati za mkakati wa kitaifa zilizotangazwa na marais wa Democrat kama vile Biden, Obama, na Clinton zilitokana na kudumisha utawala wa Marekani kupitia kile kinachoitwa nguvu laini na taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na NATO, kwa kutumia maneno ya udanganyifu kama demokrasia na haki za binadamu. Kulingana na hati ya mkakati wa kitaifa wa Democrat, Amerika ni polisi wa dunia, na ingawa dori hii ina gharama na majukumu, wanaona haya kama gharama muhimu ya kulipa ili kuhakikisha mwendelezo wa mfumo wa kilimwengu wa Marekani na upanuzi wa ushawishi wake wa kibeberu.

Hata hivyo, katika mikakati ya Republican, kama inavyoonekana katika hati za Nixon na Trump, mantiki hiyo inatofautiana. Wanawataka washirika walipie ulinzi wa Amerika na mwavuli wa usalama inayotoa. Hili lilidhihirika wazi katika hati ya Trump ya 2025 chini ya kichwa kidogo “Kushirikiana Mizigo na Kubadilishana Mizigo,” ambayo ilizilazimisha nchi za NATO “kutumia asilimia 5 ya Pato la Taifa kwa ulinzi” (Mkakati wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani 2025, https://www.whitehouse.gov/wp-content/uploads/2025/12/2025-National-Security-Strategy.pdf; mc-doualiya.com).

Kama inavyoonekana, licha ya mbinu tofauti zilizotumika, njia tofauti zilizotumika, na vipaumbele vinavyobadilika kulingana na dhurufu na mabadiliko, lengo la msingi la hati za mkakati wa usalama wa kitaifa—iwe zimetolewa na Trump, Biden, Obama, Bush, Clinton, au viongozi wengine wa dola hiyo ya kikoloni—linabaki kuwa lengo moja, la kudumu: kudumisha uongozi wa kimataifa wa Amerika, kuimarisha utawala wake, na kuzuia kuibuka kwa dola yoyote inayoshindana na Marekani!

4- Kwa hivyo, hati ya mkakati iliyotangazwa na Trump haiwakilishi mabadiliko msingi katika malengo, bali ni mabadiliko katika mbinu zinazotumika kufikia malengo hayo. Kama ilivyoelezwa pia katika Jibu la Swali la tarehe 18/11/2016: (Kuhusu mabadiliko ya sera ya Marekani kuhusu masuala muhimu yaliyofanyiwa biashara katika enzi ya rais wa zamani, umbo halitarajiwi kubadilika, lakini mitindo inaweza kubadilika. Mfumo wa Marekani unadhibitiwa na taasisi tofauti tofauti, kila moja ikiwa na mamlaka yake ambayo huongezeka au kupungua... na hii inaathiri udumishaji umbo la sera ya Marekani ambalo halibadiliki kwa tofauti za mitindo.) Mwisho wa Nukuu.

5- Hili linaweza kuthibitishwa kwa kuchunguza kuibuka kwa vyama vya kisiasa vya Marekani baada ya kuundwa kwa Marekani. Vyote vina asili moja, kudumisha utawala na udhalimu wa Marekani. Vyama hivi hutofautiana tu katika mbinu zao na udhalimu wa kibinafsi.

a. Baada ya Wazungu (walowezi na watalii) kufanikiwa kuiteka Amerika, hasa Amerika Kaskazini, na kuwafanya watumwa wakaazi wake wa asili, Wamarekani Wanati, walianza kufanya kazi ili kuunda dola. Kulingana na Wikipedia, [Makoloni Kumi na Tatu yalikuwa makoloni ya Uingereza kwenye pwani ya Atlantiki ya Amerika Kaskazini ambayo yalijitenga na Ufalme wa Uingereza katika Vita vya Mapinduzi vya Marekani (1775–1783), na kuungana kuunda Marekani]. Kongamano la Philadelphia lilitabanni Katiba ya sasa ya Marekani mnamo 17/9/1787, na iliidhinishwa mwaka uliofuata, 1788, na kufanya majimbo haya kuwa sehemu ya jamhuri moja yenye serikali kuu. Baadaye, Marekani ilipata maeneo kutoka Ufaransa, Uhispania, Mexico, na Urusi, na kuiunganisha Jamhuri ya Texas na Hawaii. Jamhuri hiyo ilianzishwa rasmi mwaka uliofuata, mnamo 1789, Marekani. George Washington alikuwa Rais wa kwanza wa Marekani (1789-1797).

b. Chama cha Democratic-Republican kilitokana na kundi katika Bunge la Congress lililokuwa na wapinzani wa sera za kati za Alexander Hamilton, ambaye alihudumu kama Waziri wa Hazina chini ya Rais George Washington

c. Chama cha Democratic-Republican kilidumu hadi 1828, wakati Chama cha Democratic cha sasa kiliundwa na wafuasi wa Andrew Jackson. Chama cha sasa cha Republican kilianzishwa mwaka wa 1854. Abraham Lincoln akawa rais wa kwanza wa Republican wa Marekani mwaka wa 1865...

6- Kwa hivyo, vyama hivi vina asili moja: kulazimisha utawala wa Marekani. Vinatofautiana tu katika mbinu zao, kiwango chao cha ujanja, na kiwango cha udhalimu wao binafsi. Tofauti hizo hazizidi nukta hizi tatu.

Kwa mfano, hati mpya ya kimkakati iliyotangazwa na Trump ni mfano wa kiburi zaidi wa tabia ya cowboy. Kama tulivyosema hapo awali, huku Wanademocrat, mithili ya mbweha, wakitoa sumu katika sura ya utamu wa uongo (chini ya pazia la demokrasia, haki za binadamu, na upole wa kidiplomasia), Wanarepublican wanalazimisha sumu kama ilivyo, wakisaga meno yao na kuashiria nguvu kali. Kauli mbiu ya Trump, “Amerika Kwanza,” kiuhalisia si chochote ila sera ya vitisho ya kikoloni, hata kwa washirika, kupitia kulazimisha ushuru: “Lipa pesa kwa ajili ya ulinzi”

7- Kwa hivyo, baada ya kuchunguza kwa undani mikakati ya Trump na Biden, inakuwa wazi kwamba tofauti pekee iko katika mtindo, ujanja, na kiwango cha udhalimu wa kibinafsi. Ingawa kile tulichotaja hapo juu kinaonyesha hili, mikakati yote miwili ilishughulikia masuala kadhaa ya kimataifa, ambayo mengi yanafanana sana katika mitazamo yao, kama vile Ulaya na China. Baadhi ya masuala, kama vile Ulimwengu wa Magharibi, yanaonyesha tofauti katika mtindo, ujanja, na udhalimu wa kibinafsi, huku mengine, kama vile Mashariki ya Kati, yana sifa ya mbinu ya pamoja, ingawa ni ya chuki, na ya njama. Tutataja kwa ufupi yaliyosemwa katika mkakati wa Biden na kisha Trump kuhusu Ulimwengu wa Magharibi na Mashariki ya Kati:

A. Ulimwengu wa Magharibi: Kwa sababu Mafundisho ya Monroe yanahusu eneo hili, tutataja jambo fulani kuhusu Monroe na mafundisho yake:

(Alikuwa Rais wa tano wa Marekani, akihudumu kuanzia 1817 hadi 1825. Alipokea jimbo la Florida kutawala mwaka wa 1819. Mnamo 1823, alitangaza Mafundisho ya Monroe, ambapo alionyesha upinzani wa Marekani kwa uingiliaji wowote wa Ulaya katika masuala ya Amerika. Hili lilisemwa katika tangazo lililotolewa na Rais James Monroe katika barua aliyoiwasilisha kwa Bunge la Congress la Marekani mnamo 2 Disemba 1823. Mafundisho ya Monroe yalitoa wito wa kudhamini uhuru wa mataifa yote katika Ulimwengu wa Magharibi dhidi ya uingiliaji kati wa Ulaya uliolenga kuwakandamiza au kuingilia uhuru wao. (Wikipedia, imebadilishwa kidogo))

Marais wa Marekani waliofuata walifuata mkondo huo katika kutekeleza hilo, ingawa kwa njia na viwango tofauti vya uovu na udhalimu. Tutataja kwa ufupi kile kilichotolewa na Biden na Trump katika mikakati yao husika ili kuonyesha tofauti kati yao.

* Mkakati wa Biden unaonyesha kwamba eneo hili (ndilo lenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Marekani, huku biashara ya kila mwaka ikifikia dolari trilioni 1.9, pamoja na maadili ya pamoja, mila za kidemokrasia, na mafungamano ya kifamilia. Mkakati huu unaona ni muhimu kwa Marekani kufufua biashara zake Amerika. Mkakati wa Biden pia unaonyesha kwamba Marekani itaendelea kuboresha miundombinu yake ya mpakani na kujenga mfumo wa uhamiaji wa haki, utaratibu, na utu na nchi za eneo hilo. Pia itaendelea na dhamira yake ya kupanua njia za kisheria za uhamiaji na kupambana na ulanguzi). Mkakati huu hauruhusu dola nyengine yoyote kuu kuwa na ushawishi thabiti unaoshindana au kuzidi ushawishi wa Marekani, bali hutumia udanganyifu na mbinu chafu kwa kutumia demokrasia na haki za binadamu... na hutumia hatua za kijeshi kama suluhisho la mwisho tu, sio kama hatua ya kwanza.

* Kuhusu mkakati wa Trump, unaanza na vitisho vya hatua za kijeshi, hata kama vitisho hivyo havitatekelezwa kamwe! Mkakati wa Trump umejaa kiburi, na vitisho. Mkakati wake (kwa maneno mengine) unajumuisha yafuatayo: [...(Kutumia Mafundisho ya Monroe kulinda usalama wa Amerika na kuregesha udhibiti wake juu ya Ulimwengu wa Magharibi—Amerika yenyewe, Canada, na Amerika Kusini—na kuzuia dola za kigeni kupeleka vikosi huko)... na analiona kama “eneo la Marekani pekee”]... Kwa hivyo, Trump aliiomba Canada ijiunge, na kuifanya kuwa jimbo la 51. Aliitishia Panama kufuta makubaliano yake na China, na Panama ikatii. Pia alianzisha shambulizi mnamo 3/1/2026 dhidi ya Venezuela, akipiga bomu mji mkuu wake Caracas, na rais wake, Maduro, na mkewe walikamatwa kwa kitendo cha kiburi kilichojaa ukoloni wa kale na wa kuchukiza! Muamala huu kwa Ulimwengu wa Magharibi uliitwa Mafundisho ya Trump, nyongeza ya Mafundisho ya Monroe. Trump hata alipanua vitisho vyake kwa Greenland, eneo linalomilikiwa na Denmark, mwanachama wa NATO! Udhalimu wa Trump ni dhahiri!!

B- Suala la Mashariki ya Kati, kama tulivyosema hapo awali (ikiwemo Mashariki ya Kati, ambapo walikula njama dhidi yake na watu wake), mikakati hiyo miwili haikuridhika na kile walichokieleza kuhusu kuunga mkono umbile la Kiyahudi na kupanua uhalalishaji mahusiano kati yake na watawala, wala kupora utajiri wa Ummah, haswa mafuta ya Ghuba na rasilimali zengine, wala kutawala urambazaji kupitia njia za maji za Mashariki ya Kati, ikijumuisha Mlango-Bahari wa Hormuz na Bab el-Mandeb. Hazikuishia hapo, bali pia zilieleza kupambana na ugaidi, ambao, kwa ufahamu wao mbaya, ni Uislamu na utawala wa Kiislamu. Trump anasema katika mkakati wake wa Mashariki ya Kati: “...kwamba eneo hilo lisiwe kihifadhi au msafirishaji wa ugaidi dhidi ya maslahi ya Marekani au ardhi ya Marekani, na kwamba Israel ibaki salama.” Biden anasema katika mkakati wake: “kukabiliana na vitisho vya kigaidi...” Nia ya yote haya ni kutishia Uislamu, fikra msingi ya watu wa eneo hilo, kwa kuwa wakaazi wake ni Waislamu wanaojitahidi kusimamisha dola yao kulingana na itikadi yao ya Kiislamu, kukomboa ardhi zao kutoka kwa utawala wa Marekani na Magharibi, kupindua serikali zao za kitumwa, na kuliondoa umbile la Kizayuni. Sio tu kuhusu kuzika makubaliano ya uhalalishaji mahusiano.

8- Kwa kumalizia, uti wa mgongo na kiini cha hati za “Mkakati wa Usalama wa Kitaifa” zilizotangazwa na marais wa Marekani tangu Vita vya Pili vya Dunia zimebaki kuwa thabiti na zisizobadilika. Kinacho badilika ni mbinu za utekelezaji, uovu, na udhalimu wa kibinafsi katika kulazimisha, kulinda, na kuendeleza utawala wa Marekani, kupigana na Uislamu na watu wake, na kufanya kila wawezalo kuzuia kusimamishwa kwa dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Lakini hukumu yao ni ovu kiasi gani! Khilafah Rashida inawakosesha usingizi, hata kwa kutaja jina lake tu. Kama Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa, Tulsi Gabbard, alivyosema siku chache zilizopita mnamo 21/12/2025, “fikra hii ya Kiislamu ni tishio la moja kwa moja kwa uhuru wetu kwa sababu, kimsingi, ni fikra ya kisiasa inayotaka kuunda Khilafah ya kimataifa.” Na tunasema: [مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ] “Kufeni kwa chuki yenu!” [Aal-i-Imran: 119]. Kwani Ummah wa Kiislamu utainuka na kusimamisha dola yake, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), baada ya utawala huu dhalimu tunaoishi chini yake.

«...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ»

…Kisha utakuwepo utawala wa kidhalimu, na utadumu kwa muda wote ambao Mwenyezi Mungu atataka udumu. Kisha atauondoa atakapotaka kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.’ Kisha akakaa kimya” (Imesimuliwa na Ahmad). Na wakati huo, hatima ya Trump dhalimu na wasaidizi wake haitakuwa tofauti na hatima ya Kisra na Kaisari baada ya kusimamishwa kwa Khilafah.

[بَلَاغٌ فَهَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الْفَاسِقُونَ]

“Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine isipo kuwa walio waovu tu?” [Al-Ahqaf: 35].

25 Rajab 1447 H

14/1/2026 M

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.